Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
Jihadharini na Wizi wa Mtandao wa Vodacom ambao umeingia kwa kasi sana. Wizi huu unahusisha matumizi ya Mpesa. Imetokea Jana kwa rafiki yangu kaingiziwa laki moja kwenye Mpesa yake na MTU asiyemjua, then huyo MTU akampigia kutoka namba ya Voda 0745195033 kuwa amekosea hivyo azirudishe hizo hela, akampa namba ya kutuma kwa DANIEL JOSEPH NO 0744880618. Huyu rafikiyangu kweli kucheki balance yake akakuta ana laki zaidi, basi akairusha kwa yule MTU kama alivyoombwa. Baadae alipocheki balance akakuta ni zero, hela zake zote zimeondoka!!!
AKAJARIBU kupika Simu zote mbili hazikuwa na majibu. Baadae akapokea Simu toka kwa dada akisema kuwa yeye ni Vodacom customer care no 25576670, akamweleza eti kashibiwa na akamwambia asihangaike kwenda Voda hawatamsaidia.
Kwahiyo jamani Jihadharini na Wizi huu wa Mtandao wa Vodacom, inaonesha wafanyakazi wa Voda wanahusika.