Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,505
WASHAURI:
Hawa ndio watu muhimu kabisa katika Taifa. Ni watu ambao huonesha njia wakati wa mkwamo. Hutoa ufumbuzi wa mambo magumu na kufanya mambo yaendelee. Uzoefu, elimu na hekima zao ni nyenzo muhimu katika maendeleo ya jamii wanamoishi.
WAKOSOAJI.
Ni watu muhimu kwa kiwango kikubwa pia. Wakosoaji hustua akili na fikra za watawala na kuwafanya kufikiri zaidi ya mara moja juu ya maamuzi yao. Wakosoaji ni watu wanaofikiri tofauti au wanaopenda kufikiri tofauti ili mradi waonekane wana fikra mpya/fikra mbadala. Wakosoaji huonesha zaidi umuhimu pale wanapokosoa na kutoa mapendekezo, la bila kutoa mapendekezo, umuhimu wao hupotea.
WASIFIAJI.
Ni watu muhimu wakati ambapo hakuna changamoto kwa sababu lengo hasa la kusifia ni kufurahisha na kujifurahisha. Mara nyingi wasifiaji ni watu wasiofikiri zaidi ya msifiwa. Wao fikra zao kutegemea sana matendo ya mtu wanayemsifia. Wasifiaji hawana nafasi katika kuibua fikra mpya au mawazo mbadala. Maana yake ni kuwa kusifiwa mara nyingi kunamfanya mtu kuenenda katika matendo/njia ileile bila uangalifu. Kuenenda katika namna ileile maana yake ni kubaki mahala palepale na kufanya yaleyale kwa sababu ya kusifiwa.
WATU Muhimu kabisa ni Washauri, wanaofuatia kwa umuhimu ni wakosoaji, wa mwisho kwa umuhimu ni wasifiaji.