Jifunze siri ya kutenda miujiza (Mfano kutembea juu ya maji, kupaa angani n. k)

Bennie 369

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
713
529
Kuna shuhuda za watu walioonekana au kusikika wamefanya vitu ambavyo huonekana ni miujiza machoni mwa watu wengi... mfano kutembea juu ya maji,kupaa angani n. k. ambavyo tunaweza kusema ni vitu vinavyopingana na gravitation force lakini Kuna watu wameweza kuvifanya mfano Jesus christ, chriss Angel,Dynamo n. k
Je unaijua siri ya kutenda miujiza hii?... hata wewe ukiamua unaweza,,, ila kuna vitu viwili tu vya kuzingatia, ambavyo ni kuwa na MATUMAINI pamoja na IMANI ya kile utakachofanya .

JINSI YA KUFANYA.
Kwa watu ambao wana uwezo wa kutoka nje ya mwili au kufanya Astral projection hili swala litakuwa rahisi sana kwao kufanikisha
Hatua za kufuata ...
1.lala kwa ubavu wa kushoto huku kichwa chako kikiwa kimelalia kiganja chako cha mkono wa kushoto
2.jilegeze mpaka uwe kwenye hali ya kusinzia (lakini usilale usingizi )
3.jitahidi kuzuia au kutokuzingatia taswira au mawazo yeyote yanayokuja kwenye mawazo yako
4.elekeza uzingativu wa mawazo yako katika hali ya ndoto, yaani kipindi unachoelekea kulala usingizi hisi kama upo kwenye ndoto
5.unapofikia hatua ya kuhisi kama unataka kulala usingizi mzito, fuata hatua zifuatazo ...
Amka na ukae kitandani au sehemu uliyokuwa umelala zingatia kuwa makini kipindi unachoamka kwa maana kwamba inabidi uinuke au kuamka katika hali ya mtu anayeota usingizini, kwa sababu uwezo au nguvu zote zinafanyika katika hali ya kuwa katika ndoto, inuka na usimame wima kwa miguu na pia zingatia kuwa makini kipindi unaposimama ili usiweze kusimama/kurudi katika hali ya ukawaida kwa maana kwamba unakuwa kama mtu anaye weweseka ila unachokifanya unakielewa ... .. . sasa jaribu kuruka juu kidogo ukiwa na lengo la kuelea hewani kama unataka kupaa, kama ukiona unavyoruka huelei hewani lala tena halafu uzirudie hizo hatua.
ili jambo Kuna watakaoweza kulifanikisha kwa mara moja, wengine inaweza kuwachukua siku,wiki , mwezi na hata mwaka kulifanikisha... ila cha mhimu ni kuwa na MATUMAINI pamoja na IMANI ya kuwa unachokifanya kinawezekanika na hii itakufanya ufanikishe hili jambo kwa mda mfupi tu .
Kwa watakao fikia hatua ya kuruka na kuelea hewani watakuwa wamefanikiwa kuwa katika hali ya jinna state hivo wataweza kufanya chochote mfano kutembea juu ya maji, kuruka hewani au kuwa katika astral plane katika physical body na hii ni kwa sababu unakuwa katika jinna State , hivo utaweza kwenda mahali popote kwa mda mfupi (ikumbukwe kuwa katika astral plane time and space do not exist because everthing is eternal "now " and eternal "present ".
 

Attachments

  • IMG-20160218-WA0019.jpg
    IMG-20160218-WA0019.jpg
    7.9 KB · Views: 257
Uturushie video clip yako mwalimu au huyo aliyekufundisha ili tukuze hiyo imani. Maana kwa hiyo mechanism Unaweza kujirecord.
Tutakuwa umesaidia sana.
Natanguliza shukrani lkn ukumbuke yesu akujitesa hivyo ili atembee juu ya maji.
 
Uturushie video clip yako mwalimu au huyo aliyekufundisha ili tukuze hiyo imani. Maana kwa hiyo mechanism Unaweza kujirecord.
Tutakuwa umesaidia sana.
Natanguliza shukrani lkn ukumbuke yesu akujitesa hivyo ili atembee juu ya maji.
nashukuru kwa ushauri wako ndugu ...
 
Umeanza lini na umeruka mara ngapi? Usilinganishe aliyoyafanya Yesu Kristu na mambo yafanywayo na wanadamu.
nimeanza mda sana na nimeruka mara nyingi sana ......kuhusu kulinganisha hata yesu mwenyewe alisema ukiwa na IMANI utafanya zaidi hata kuliko aliyoyafanya yeye
 
Back
Top Bottom