Jifunze namna ya kutumia Tsh 300,000 kama mtaji wa kufugia kuku

As Salafiyyu91

JF-Expert Member
Jan 11, 2014
2,537
2,530
farms.jpg

Wakuu habari zenu naamini wengi wetu tutakuwa ni wazima na wale wagonjwa tuzidi kuwaombea ili warejee katika hali yao ya kawaida

Katika pitapita zangu nmekutana na post moja ikionyesha mchanganuo wa kutumia Laki Tatu kama mtaji wa kuanzia kufugia kuku nikaona sio vibaya nikaja kushare na Nyinyi ili sote tupate Faida.

====
Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanaotaga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu (300) au na zaidi kama unataka.

Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.Tafuta sehemu ya uhakika na nunua kuku wenye matunzo na kinga ili wasipatwe na magonjwa na wenye afya nzuri.

Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.

Usinunue kuku kabla hujaandaa banda la kutosha kulingana na idadi ya kuku na kwa ajili ya badae kwa kuwa mradi utaongezeka kadri siku zinavyoenda na Chakula.

Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

Mchanganuo Wa 69500 ni:-
- Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.

- Paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.

- Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500

- Layer's consetraite kilo 25 kifuko. = 21500

Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.

Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300. Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.

TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.

Mchanganuo wake

Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.
Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500

Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wa kutaga.

Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.

Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.

Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200.

Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe. Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.Kumbuka kujibana ili kuongeza banda.

====

Nawasilisha
 
Asante Sana mkuu
kwa taarifa nzuri kuhusu ufugaji
wa kuku
Kwa mtaji huu ni rahisi kuanzisha mradi tena sio lazma ukakope kwenye Bank au Saccos unaweza muonyesha ndugu yako mwenye kauwezo akakupatia mtaji
 
Hakuna uhalisia hapa kuna mambo mengi hayajaingizwa kwenye huo mchanganuo ambayo ni muhimu. Kuacha kujumuisha mambo yote kwenye mradi wa aina yoyote ile ni kutengeneza 'mama wa mabomu' ambalo litapelekea kuulipua mradi yaani kufa kwa mradi.
Mkuu kwa mfano mambo gani yamekosekana ?
 
1. ulinzi wa hao kuku inakuwaje? 2. usafiri kwa baadhi ya vitu mfano hicho chakula, vifaa vya ujenzi 3. gharama za maji na umeme 4 banda lenye kiwango cha chini laweza kupelekea kuku kuliwa na vicheche, 5. etc.

Kuna kanuni za namna ya kupanga namna kuanzisha mradi au biashara. Kanuni hizo zimegawanyisha gharama za mradi kwa namna kuu tatu: capital, fixed/ overhead and direct/ variable cost.

Ukiona laki tatu inatosha kama unavyosema, lazima kutakuwa na gharama ambazo umeingia in kind (kubeba mabati au kukata miti ya kujengea mwenyewe), au bila kujua mfano ankara za maji na umeme.

Ila kodi ya vyakula vya kuku kwa 2017/ 18 imeshuka.
 
1. ulinzi wa hao kuku inakuwaje? 2. usafiri kwa baadhi ya vitu mfano hicho chakula, vifaa vya ujenzi 3. gharama za maji na umeme 4. banda lenye kiwango cha chini laweza kupelekea kuku kuliwa na vicheche, 5. etc.

Kuna kanuni za namna ya kupanga namna kuanzisha mradi au biashara. Kanuni hizo zimegawanyisha gharama za mradi kwa namna kuu tatu: capital, fixed/ overhead and direct/ variable cost.

Ukiona laki tatu inatosha kama unavyosema, lazima kutakuwa na gharama ambazo umeingia in kind (kubeba mabati au kukata miti ya kujengea mwenyewe), au bila kujua mfano ankara za maji na umeme.

Ila kodi ya vyakula vya kuku kwa 2017/ 18 imeshuka.
Ni kweli unayosema lakini jamaa ametoa mwangaza wa kuanzia huwezi ukaanza mradi pasi na kuwa na changomoto ndo kama hizo ulizo zieleza lakini ukithubutu kufanya naamini utajua jinsi ya kutatua changamoto zitakokuwa zinakukabili
 
Hakuna uhalisia hapa kuna mambo mengi hayajaingizwa kwenye huo mchanganuo ambayo ni muhimu. Kuacha kujumuisha mambo yote kwenye mradi wa aina yoyote ile ni kutengeneza 'mama wa mabomu' ambalo litapelekea kuulipua mradi yaani kufa kwa mradi.
ukisema kuna mambo hayajajumuishwa unatakiwa utueleze ni yapi,vinginevyo kaa kimya kama huna point jamaa kaeleza vizuri
 
Wakuu habari zenu naamini wengi wetu tutakuwa ni wazima na wale wagonjwa tuzidi kuwaombea ili warejee katika hali yao ya kawaida

Katika pitapita zangu nmekutana na post moja ikionyesha mchanganuo wa kutumia Laki Tatu kama mtaji wa kuanzia kufugia kuku nikaona sio vibaya nikaja kushare na Nyinyi ili sote tupate Faida.

====
Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanaotaga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu (300) au na zaidi kama unataka.

Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.Tafuta sehemu ya uhakika na nunua kuku wenye matunzo na kinga ili wasipatwe na magonjwa na wenye afya nzuri.

Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.

Usinunue kuku kabla hujaandaa banda la kutosha kulingana na idadi ya kuku na kwa ajili ya badae kwa kuwa mradi utaongezeka kadri siku zinavyoenda na Chakula.

Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

Mchanganuo Wa 69500 ni:-
- Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.

- Paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.

- Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500

- Layer's consetraite kilo 25 kifuko. = 21500

Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.

Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300. Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.

TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.

Mchanganuo wake

Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.
Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500

Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wa kutaga.

Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.

Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.

Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200.

Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe. Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.Kumbuka kujibana ili kuongeza banda.

====

Nawasilisha
Fungua hii pdf usome mchanganuo mzuri namna ya ufugaji bora wa kuku
 
Attachments

  • MicrosoftWordkanunizaufugajiborawami.pdf
    86.6 KB · Views: 1,517
too theoretical! umejenga banda moja na hela imeisha, banda la vifaranga liko wapi? au utawalaza na mama zao? kuku wa kienyeji kutaga kwa kiwango cha 80%, we utapata nishani ya ufugaji bora.
 
Gud aisee ila haujafanya hitimisho kuwa na kuku wengi tu sio faida maana haujawapata buure

Malizia hapo wakishakua mia mbili unapataje faida.

Yaani.
Mauzo-manunuzi=faida.
 
Hivi kuku hawa ni wa kienyeji au ni layers?

Kama ni wakienyeji, huwezi kuzalisha mayai 240 kwa mwezi kwa kuku 8. Hivi kuna kuku wa kienyeji anayeweza kutaga Mayai 30 mfululizo?? Yaani mwezi mzima anataga tuuuu mpaka yanafikia mayai 30!!

Nipe na mimi hiyo mbegu aisee, kuku nnaowafuga wanataga Mayai 12 hadi 15 baada ya hapo wanaacha kutaga na kuhitaji kuatamia.

Ukiwanyang'anya mayai na kuyaweka kwenye incubator, wataendelea kukaa si chini ya siku 40 kabla kuanza kutaga tena.

Nakupongeza kwa mchanganuo mzuri lakini umewapa watu matumaini makubwa mno kuliko uhalisia,
 
mimi changamoto yangu kubwa Zaidi ni moja, vipi kwa maeneo yenye baridi kali (mf. Mufindi Iringa), mambo gani ya kuzingatia? Natamani sana kuanza kufuga lakini hii baridi naiwaza
 
Back
Top Bottom