Jifunze maajabu ya 1089

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
38,876
44,926
Nilikutana na hii nilipokua Form 5 long time ago, ila leo nimekumbuka na kujiuliza, nini chanzo cha inherent properties ilizonazo namba 1089.

1.) Andika namba yeyote yenye tarakimu tatu ambapo, namba ya kwanza ni kubwa kuliko namba ya mwisho.
Mfano: 725

2.) Iandike namba hiyo kinyume, kwa kuanza na tarakimu ya mwisho hadi ya kwanza. Kwa mfano wetu hapo juu tutaandika : 527

3.) Chukua hiyo namba ya kwanza (725) utoe na kinyume chake (527), kwa huu mfano wetu ni : 725 - 527 , tunapata jibu ni: 198

4.) Andika jibu ulilopta kwenye hatua ya tatu (198) kwa kinyume, kuanzia tarakimu ya mwisho hadi ya kwanza, kwa mfano wetu tutaandika : 891

5.) Sasa chukua jibu la hatua ya nne (891) ujumlishe na jibu la hatua ya tatu (198). Kwa mfano wetu itakua 891 + 198, jibu tunalopata ni 1089 !

Kwa namba yeyote yenye tarakimu tatu, ambapo namba ya kwanza ni kubwa kuliko na ya mwisho, basi ni lazima ukifuta hiyo procedure upate jibu ni 1089!

In case kwenye hatua ya tatu ukapata jibu ni namba yenye tarakimu mbili, basi ongezea sifuri.

Je, hii namba 1089 ina nini hasa, inherently!
 
Funguka mkuu Manake wazungu wao wanaamini Friday 13 ndio siku ya mikosi. Sijui hio 13 pekee yake ndio kwanza nimesoma hapa kwako.
Mkuu si hilo tu, ni story ndefu ya baadhi ya scenarios kama 3 zilizonitokea na kukumbushwa hiyo namba.

Moja kubwa Ilianza Ijumaa moja ya mwaka 1997, tukiwa tumetoroka shule na kwenda kuoga mtoni huko Arusha (Mto themi) tukiwa watano na marafiki zangu...akazama rafiki yetu mmoja majini (Marehemu sasa) na kupanda juu na alichosema mbele yangu ni "Niagie kwa mama"

Nikakumbuka nilichoambiwa siku iliyopita na Mzee mmoja wa India (Mgoha) alikuwa akiishi karibu na shule ya msingi Sanawari kwa miaka mingi sana (waliosoma sanawari watakuwa wanawafahamu hawa)

Aliniambia kesho ni siku mbaya kushika mshumaa au kujiangalia katika kioo asubuhi. Pia ni siku mbaya kuithamini namba hii (akaniandikia juu ya daftari langu)

Maajabu makubwa ni ile siku ya taarifa ya msiba kufika pale shuleni, yule Mzee wa kihindi pia alikuja akaniangalia akaniambia hukumwambia rafiki yako?

Kiukweli nikawa kama naota na nikakumbuka mambo mengi aliyokuwa ananihadithia rafiki yangu huyo kuhusu maisha ya nyumbani kwao (tulikuwa desk 1)..

Habari ya namba 13 nikaisahau japo nlijua ina mambo, ikaja tena kudhihirika nikiwa sekondari fm four karibu na mitihani.
 
Sanawari
 
tofaut na wale wanabashiri namba kwa kukuambia jumlsha namba fulan toa namba fulan jibu fulan.

Kuna mwalimu wetu wa Math alituambia darasa zima tufilirie namba afu tundke kwny vikaratas yyote asivione.ndani ya dakka moja aliweza kututajia namba zaid ya nusu ya wanadarasa na zote zikawa sahih.
Sijajua mpk leo alitumia utaalamu gn.
Myb km kuna anayefahamu huu utaalamu aliotumia atujuze...
 
Hiyo ya kujumlisha na kutoa ni very straight forward.., ila hiyo ya mwalimu wako natamani kuijua alifanyaje.., ila kwanini hukumuuliza?
 
Sasa kwenye numerology, wanasema namba 9 ndo namba inayo guide namba zote kiujumla wake, kwa mfano katika hii namba
1089
1+0+8+9=18
1+8=9,

Alafu ukija kwenye hiyo 198, na 189 ukizi-add moja moja
Mfano: 1+9+8=18
1+8=9

Na

189
1+8+9=18
1+8=9

Ukija tena difference ya
198-189=9

Na hata ukizi-add
198+189=387
3+8+7=18
1+8=9....

Sasa kuna namba 369...hii ndo namba ambayo ina maajabu yake

Think in terms of vibration, frequency and energy- NIKOLA TESLA
 
Back
Top Bottom