Jifunze kuhusiana na 'Boss' wako vizuri

Jielewe

Member
Jan 10, 2017
39
62
Moja ya mambo yanayoweza kukusaidia kufanikiwa kazini ni namna unavyohusiana na mkubwa wako wa kazi. Huyu ni mtu anayekuongoza, anayetoa maelekezo ya nini kifanyike na wakati mwingine ndiye mwenye kauli ya mwisho kwenye taasisi, idara au ofisi unayofanya kazi.

Kwa nafasi yake, kiongozi wa kazi ni mtu mwenye mamlaka ya kufanya maamuzi yanayohusu kazi yako hata kama anaweza asiwe mwajiri wako moja kwa moja. Huyu ni mkuu wa ofisi, idara, kitengo, kampuni au taasisi unayofanyia kazi. Ndiye mtu anayekusimamia na kupokea taarifa za utendaji wako na labda kuzipeleka kwenye mamlaka za juu.

Usipoelewa namna gani unaweza kuishi na mtu mwenye mamlaka juu yako, unaweza kujiingiza kwenye matatizo makubwa yanayoweza kukugharimu. Nawafahamu watu kadhaa wenye weledi, uzoefu na ujuzi mkubwa kazini, lakini wakijikuta wakipoteza kazi zao kwa sababu ya kutokujua namna ya kufanya kazi na wakubwa wao kazini.

Ingawa ni kweli wapo viongozi wanaokosa sifa za uongozi na hivyo kuwa sababu ya misuguano kazini, bado unaweza kujifunza namna ya kupunguza migogoro isiyo na ulazima katika mazingira ya kazi.

Sambamba na bidii na ufanisi wako wa kazi ambao si sehemu ya makala haya, makala haya yanaangazia masuala matatu makubwa: heshima kwa anayekuongoza, kujua namna ya kumshauri na kuepuka mashindano yasiyo na sababu. Bonyeza hapa kujifunza zaidi.
 
Back
Top Bottom