jifunze jinsi ya kutengeneza artifical colostrum (maziwa ya kwanza baada ya kujifungua)

theriogenology

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
8,748
15,669
Wasalamu wa Jf natumaini wote mu wazima na mnaendelea vyema na shughuli mbalimbali za kulijenga taifa.... bila kupoteza wakati kama kichwa cha habari kinapojieleza hapo juu twende moja moja kwenye mada.

1. kwanza kabisa colostrum ni nini?
Colostrum ni maziwa ya mara ya kwanza anayozalisha na kuyatoa mama baada ya kujifungua, kwa muonekano yanakuwa na rangi ya manjano na maziwa haya yanakuwa na kiwango kikubwa cha albumin na globulin tofouti na maziwa ya kawaida. Kwa kifupi tunaweza sema colostrum ni mchanganiyiko wa virutubisho mbalimbali ambavyo vinamuwezesha mtoto aliezaliwa kuishi katika mazingira mapya tofouti na mazingira yale ya tumboni mwa mama yake.
Maziwa haya huzalishwa kwa muda mfupi na kadili mtoto anavyonyonya ndivyo maziwa haya hupungua na kubadilika na kuwa maziwa ya kawaida.

2. Umuhimu wa colostrum kwa mtoto mchanga
> Humpatia mtoto kinga tulivu (Passive immunity) ambayo humkinga mtoto kutoka kwa mawakala wa viambukizi kama virusi, bakteria na fangasi.
> Maziwa haya huwa na virutubisho mbalimbali vingi kuliko maziwa ya kawaida ambavyo humsaidia mtoto katika ukuaji wake.
> Hutumika kama kilainishi (Laxative agent) ambacho humsaidia mtoto kutoa kinyesi chake.

3. Mchanganyo wa colostrum
  • Mchanganyo wa colostrum unahitaji vitu vifuatavyo ;
> Maziwa ya kawaida ( whole milk) kiasi cha lita moja ( 1litre)
> Maji ya uvuguuvugu ( warm water) kiasi cha nusu lita ( half aliter)
> Kiini cha yai moja ( egg yolk from one egg)
> Castrol oil ( vijiko viwili vya chai or two tea spoons)
> Fish oil (kijko kimoja cha chai or one tea spoon)

4. Mambo ya kuzingatia wakati wa kutengeneza colostrum
Colostrum yafaa kutengenezwa katika mazingira na vyombo safi na salama ili kuepusha maambukizi kwenda kwa mtoto na pia yafaa kutumia majia ya uvuguvugu yenye nyuzi joto 37 sawasawa na joto halisi la binadamu.
 
Back
Top Bottom