prumpeti
JF-Expert Member
- Feb 28, 2022
- 1,023
- 2,320
Ni matumaini mko salama.
Leo nataka kwa pamoja tupeane mawazo na ushauri katika swala zima la (MIKOPO) hasa ya kuendesha biashara.
Kwa namna moja kila mtu amewahi kukopa bila kujali kiasi gani ila ni mkopo na wengi wetu lengu kuu huwa ni kuanzisha biashara au kuendeleza biashara. Hivyo basi kila mtu anajua mazuri na mabaya ya pesa za mikopo kwenye biashara.
Mimi tokea nimeanza biashara mwaka 2017 kwa miaka 6 yote sijawahi pitisha hata mwezi mmoja bila kuwa na rejesho la mkopo kwa uzoefu wangu naweza kusema imenisaidia pakubwa mana kwa utafutaji wangu isingekuwa hii mikopo ningesharudi kijijini.
Watu wengi wanachukulia mikopo kama shetani mfilisi sijui wao huwa wanaitumia vipi hasa? labda watatupa changamoto zake hapa..
Labda nibainishe mambo muhimu unayopaswa kuzingatia kabla na baada ya kuchukua mkopo.
1.Usichukue mkopo kabla ya kuwa na mpango mzuri wa nini utafanya baada ya kupata huo mkopo.
2.Kabla ya kuchukua mkopo hakikisha una uwezo wa kupata pesa za rejesho ikiwa biashara unayoenda anzisha itakwama.
3.Usitumie pesa ya mkopo nnje ya mipango uliyojiwekea mwanzo.
4.Usichukue pesa nyingi sana ili usipate shida ya kupata rejesho la kila mwezi.
5.Chukua mkopo kwenye taasisi ambazo zinafanya shughuli zake kihalali ili kuepuka kuongezewa riba kubwa ambayo mara nyingi ndio chanzo cha kukwama kwa wakopaji wengi mpaka kufikia kusema pesa za mkopo ni za majini.
KOPA KISTAARABU TUMIA KISTAARABU.[emoji16]