jifunze hapa mkuu

jifunze hapa mkuu

nina nchi sita

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
269
Reaction score
146
Faridi akiwa na mchepuko wake katika bar moja maarufu, Mara sim yake inaita. Ni doctor ambaye familia zao zilikuwa na urafiki mkubwa ndiye alikiwa akimpigia. Faridi baada ya kupokea simu haamini anachoambiwa. Ati mkwe kafa anahitajika nyumbani haraka. !

Faridi haamini maskio yake anahisi yupo ndotoni, na ataamka hivi punde. Jeska ambaye ndiye mchepuko wake anajaribu kumtuliza bila mafanikio.

Faridi anachomoka mbio mpaka sehemu alipo paki gari. Anaingia ndani ya gari huku Watu wanamshangaa na zaidi wanaushangaa utoaji wake gari katika parking. Na spidi anayo ondoka nayo kila mtu haamini kama atafika salama
*********************_*********
*****************_*******
Faridi anakanyaga mafuta zaidi na zaidi kila palipo na uwezekano. Anakumbuka hii ni wiki ya pili sasa hajarudi nyumbani, na amekuwa akila bata na michepuko yake bila kuikumbuka familia yake. Majibu mabaya aliyo kuwa anamjibu mke wake yanajirudia kichwani kwake. "Umeshachoka wewe saivi lea watoto hapa nyumbani acha nikachangamshe damu kwa vitoto vipya. Faridi akakumbuka kwamba kuchoka kwa mkewe kunatokana na yeye mwenyewe kutomhudumia vizuri na majukumu makubwa ya kulea familia aliyonayo. Machozi yakamtirika akatamani aamke katika usingizi ili akatoshe ndoto nzito aliyokuwa anaota lkn haikuwezekana. Ni Jana tu mkewe alipompigia cm akapokea baada ya kutopokea kwa mda mrefu. Mkewe alipo taka kujua yukowapi akafoka saana kwenye simu akimtuhum mkewe kwa kukosa kumuamini.

Faridi hakuamini kwamba huu ndio mwisho wa kumuona mkewe. Mwisho mbaya kabisa, na hajui ni mwisho uliojenga picha gani kwa kwa wanae kwani mala nyingi walimshudia baba yao akimpiga mama yao mbele yao

************************†************
********†*************

Faridi hukuona umuhim wa kusubiri geti lifunguliwe, alishuka kwenye gari na kufungua geti akajitosa ndani. Akamkuta dokta akimsubiri uwani. Faridi huku akilia akauliza, "yuko wapi mke wangu kipenzi". Dokta akamuonyesha ishara aingie ndani

Faridi alipo ingia ndani hakuamini macho yake alipo muona mkewe akiwa na mke wa dokta(mtaalam wa saikolojia) .faridi akamfuata mkewe na kumkumbatia kwa nguvu huku akilia na kumuomba radhi kwa makosa yake yote. Mkewe pia akamkumbatia faridia huku akilia

Dokta akawatazama wawili hao huku akisema,"poleni sana na pia hongereni kwa kugundua upendo uliopo miongoni mwenu. Faridi,tulitumia njia hii kukufanya uutambue umuhim wa mkeo. Ilikuwa njia hatari lkn salama kwa ndoa yenu

*********MWISHO*******
Tafadhali andika kitu ulichojifunza kutokana simulizi hii

Ni mimi Mme mtarajiwa wa trace mizengo pinda
 
Back
Top Bottom