Jicho

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,323
Kazi kubwa yako jicho, ni ngumu nai-husudu,
Nimefanya mchekecho, kwa ufundi na utundu,
Naamini nisemacho, kazi yako waimudu,
Jicho kazi yako ngumu, Leo nakusema wewe,

2. Huenda ni mpekecho, niliyofanya akidu,
Nili-sifiapo jicho,tumbo usifanye ndundu,
Tunza chakula kilicho, ndani usifanye pindu,
Jicho kazi yako ngumu, sifa nakupa za kweli

3. Kila wewe uonacho, Mnyama au mdudu,
Ubongo wampa hicho, ugawanye kama ladu,
Ulimi ampe hicho, kujua kama ungwadu,
Jicho kazi yako ngumu, sifa nakupa za kweli


4.kama wazi kiwekwacho,chaonwa kama kidundu,
Au kilicho maficho,hata kama vipo dundu,
Ukianza na mchakacho, utaona hadi kidu,
Jicho kazi yako ngumu, kufichua vilofichwa,

5. Ila- kini tatizacho, huchagui ka madudu,
Waona kilicho maficho,kichafu ama kibudu,
Hata haramu kilicho, kwanza ona kasha mbwedu
Jicho kazi yako ngumu, kufichua vilofichwa,


6.Vile vilivyo kificho, utachungulia tundu,
Utahangaika jicho, ukione japo bandu,
Ndo yako mapocho pocho,hata kushinda matandu,
Jicho kazi yako ngumu, kufichua vilofichwa,


7.Wengi hupanzwa na jicho, subira kutoi-mudu,
Wapatwapo mchikicho,walipoona vyekundu,
Lawamazo kochokocho, kumbe ni wao utundu,
Jicho kazi yako ngumu,chochote uone wewe,

8 Kituoni nimefika, nazikomesha nudhumu,
Yatosha naloandika, jichoni ni jahanamu,
Ashikae atashika, asoshika Si lazimu,
Jicho kazi yako ngumu,usitutie motoni,


9. Tamati ndio akhiri, na jina langu ni hili
Hamza wa Yusuf, na Barubaru ni akhili
Mtungaji mashuhuri, mpenda kusema kweli
Jicho kazi yako ngumu,usitupe majaribu, Dr Hamza Yousuf Al Naamani +974 4457 4888.Safarini isamilo Mwanza Tanzania

 
Back
Top Bottom