Jicho la tatu

Jicho la tatu

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
19,147
Reaction score
43,081
FB_IMG_1724852336811.jpg

Imeandaliwa na kuandikwa na Dokta Dotto Aliko

🗣️Tuna macho mawili ambayo Ni macho ya uongo fake eyes, lakini pia tuna jicho moja ambalo ndiyo jicho la kweli true eyes, Hivyo tuna macho matatu lakini mawili Ni ya uongo na moja Ni la ukweli nalo siyo lingine Ila Ni lile lililopo Kati Kati yaa paji la uso.

👁️Iangalie Nazi moja Kati ya bidhaa ambayo inamaajabu sana, siko hapa kuzungumzia maajabu ya Nazi Ila Nazi Ni mfano mzuri wa hiki ninachokizungumza hapa Nazi Ina macho matatu, Kati yao mawili ya uongo na moja Ni lakweli.

✍️Jaribu kuangalia vile vitobo vitatu vya Nazi, Ni kimoja tu ndiyo ukikitoboa kinatoboka na kutoa maji Ila vile viwili Ni mfano tu wa kitobo Ila siyo vitobo, Basi ndiyo mfano wa haya macho yetu ya kifizikia na jicho la tatu.

👀Haya macho yetu Ni macho ya uongo, Kama ulivyo huu mwili wa uongo ndivyo yalivyo macho yetu, Ila Kuna jicho la kweli ambalo Ni moja tu.

👁️Nalo siyo lingine Ila Ni lile jicho ambalo lipo katika paji la uso, jicho la tatu, Hili ndiyo jicho lenye uwezo wa kukuoneshea Yale usiyoyaona.

🗣️Rejea Ile stori ya yesu anawaponya vipofu wawili bado Ni fumbo Hili hili la macho ya uongo na jicho la tatu, Wale vipofu wawili Ni macho yetu haya mawili ya kifizikia ambayo hayawezi kuona Yale Mambo ya kiroho, lakini yesu anawafunga macho yao kwa mikono yake na baada ya kuwaachia nao wanasema kwamba wanaona. Hapa Kuna SoMo lingine ambalo mnatakiwa muelewe kwamba ili tuone ya kiroho Basi milango ya kifizikia inatakiwa ifungwe.

✍️"Jicho ni taa ya mwili. Kama basi jicho lako ni zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga." Unafikili kwa Nini hapa imetumika jicho na Wala siyo macho kwa sababu haya macho mawili Ni macho ya uongo Ila jicho la kweli Ni moja.

🤔Wazee wetu walikuwa wanawapaka wanja watoto wadogo kwenye paji la uso, kwa Nini wawapake kwenye paji la uso na Wala so sehemu nyingine, wazee wetu wanajua Nini walikuwa wanafanya na walikuwa wanafanya hivyo kwa ajili ya kumkinga mtoto na tatizo la kushtuka shtuka, je kwanini mtoto anashtuka shtuka Ni kwa sababu jicho lake la tatu liko wazi anayaona yake ambayo hayaonwi kwa macho ya kawaida Sasa akipakwa majibu au wanja inafunga jicho la tatu na kumfanya mtoto asione vitu vya kiroho na aache kushtuka shtuka.

👌Rejea siku ya jumatano ya majivu, je Yale majivu yanapakwa wapi, kwenye paji la uso, na kauli mbiu yake Ni kwamba wewe Ni mavumbi naa mavumbini utarudi, yaani unatolewa katika ukiroho na kuletwa katika Hali ya kifizikia huku nawe ukiamini kwamba kweli wewe Ni mavumbi kumbe si mavumbi wewe.

✍️ Mwalimu wako Dotto Aliko
 
Kama wazee walipaka watoto wanja kuziba jicho la tatu na jumatano ya majivu wanapaka kuziba nini?
 
👉Jicho la tatu ni alama yenye nguvu inayowakilisha kuamka kiroho na hekima ya ndani. Jicho la tatu lipo katikati ya paji la uso, mara nyingi linahusishwa na machale (intuition), ,uwezo wa akili na Ufahamu wa kina wa Ulimwengu.

👉Katika tamaduni nyingi, Jicho la tatu linachukuliwa kuwa kama lango la Ufahamu wa Juu, na hutusaidia kuweza kuona zaidi nje ya Ulimwengu huu wa mwilini na kutuwezesha kugusa nguvu za juu za kiroho zinazo tuzunguka.

👉Lakini ili kufungua nguvu ya jicho la tatu inatupasa sisi kujizoesha kuzama ndani yetu katika kina cha Ufahamu kwa uangalifu. Pia yatupasa kunyamazisha akili zetu, ili kuweza kusikiliza sauti yetu ya ndani, na kuamini uvumbuzi wetu.

👉Kwa kufanya hivyo,btutaweza kuifikia hekima yetu ya ndani na kuweza kupata Ufahamu zaidi juu ya maisha yetu wenyewe na Ulimwengu unao tuzunguka. Tunakuwa tunapatanishwa zaidi na mahitaji na matamanio yetu wenyewe, na kupitia jicho hilo tunaweza kuunganishwa kwa undani zaidi na wengine.

👉Lakini jicho la tatu si tu kwamba linatusaidia kutazama ndani yetu, pia hutuwezesha kuuona Ulimwengu katika mwanga mpya. Pia hutuwezesha kuona zaidi kwa kutupatia picha ya mwonekano wa hali ya juu wa vutu na kuweza kupata Ufahamu wa kina wa asili yao halisi. Kwamba hutuwezesha kuona mambo au vitu katika uhalisia wake wa kweli ambao wengi hawaoni.

👉Kupitia Jicho la tatu tutaweza kuona kuunganishwa kwa vitu vyote, na tutafahamu zaidi athari za matendo yetu katika Ulimwengu unao tuzunguka.

👉Kwahiyo ikiwa unahisi kuvutiwa na nguvu ya jicho la tatu, fahamu kwamba ni safari inayo faa na muhimu kupita au kuichukua kama njia yako ya maisha ya kiroho. Inatupasa tuwe na nia ya kweli ya kutaka kupata nguvu ya jicho la tatu, inatupasa tuwe wadadisi, na tuwe tayari kuzama katika kina cha Ufahamu wetu wenyewe.

👉Lakini thawabu tutakazo pata kwa kufungua nguvu ya jicho la tatu hazipimiki ni thawabu kubwa mno. -Jicho la tatu litatufanya tuwe na Ufahamu wa hali ya juu kuhusu kusudi letu na kuhisi au kujawa na hisia za hamu ya kutaka kutimiza kusudi letu, jicho la tatu litatuwezesha kupata muunganisho mkubwa wa kina katika ulimwengu unao tuzunguka, pia tutajazwa na hisia mpya za ajabu kuhusiana na Uzuri wa Ulimwengu ambapo hapo awali kabla hatukuwa na uwezo huo wa kuona uzuri wake. @everyone
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom