Jibu limepatikana

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,850
155,801
4737098.jpg

Yai na kuku kipi kilianza?
Mjadala wa miaka mingi kuhusiana na kipi kilitokea mwanzo kuku au yai? umepata jibu baada ya wanasayansi kuthibitisha kuwa kuku ndiye aliyekuwepo awali kabla ya yai.Mjadala wa miaka nenda rudi kuwa kuku na yai kipi kilitangulia duniani umepatiwa jibu na wanasayansi wa nchini Uingereza ambao wamethibitisha kuwa kuku ndiye aliyekuwepo mwanzo kabla ya yai.

Kwa kuangalia jinsi ganda la yai lilivyotokea, wanasayansi wa nchini Uingereza wanaamini wamepata jibu la mjadala huo.

Watafiti katika vyuo vikuu vya Sheffield na Warwick nchini Uingereza wamegundua kuwa protini inayoitwa ovocleidin (OC-17) ni muhimu sana katika kutengenezwa kwa gamba la yai.

Lakini protini hiyo hupatikana toka kwenye ovari ya kuku mwenye ujauzito.

Kwa maana hiyo yai lisingekuwepo kama kusingekuwa na protini ambayo inatoka kwa kuku mjamzito.

Watafiti hao waliongeza kuwa protini ya OC-17 husababisha calcium carbonate kwenye mwili wa kuku ibadilike kuwa calcite crystals ambazo ndizo hulifanya gamba gumu la yai ambalo hukilinda kiini cha yai wakati kuku anapoanza kukua ndani ya yai.

Hata hivyo wanasayansi wengine bado hawajaridhika na jibu lililotolewa kuwa kuku ndiye aliyetangulia kabla ya yai.
 
Mhh..mie sikuwahi hata siku moja kujiuliza juu ya jambo hili....ila sasa nimejua kitu fulani sina tabia ya kudadisi mambo.:A S tongue:
 
Bila hata kuumiza kichwa ni kuku kwanza halafu yai. Maanake bila kuku jike na jogoo kujamiana hakuna yai. Basi watafute pia mwanaume na mwanamke (binadamu) nani alikuwa wa kwanza?
 
Bila hata kuumiza kichwa ni kuku kwanza halafu yai. Maanake bila kuku jike na jogoo kujamiana hakuna yai. Basi watafute pia mwanaume na mwanamke (binadamu) nani alikuwa wa kwanza?

Mbona hii iko wazi kulingana na mafundisho ya dini
 
Wenzio wako kwenye sayansi zaidi kama ingekuwa wanafanya reference na mafundisho ya dini wala hupasui kichwa tena. Mungu alimuumba Adam hakuumba mimba.
[/B]Mbona hii iko wazi kulingana na mafundisho ya dini
 
Mungu aliumba kila kitu kuanzia kuku, bata...mpaka mwanadamu (Adam na Hawa/Eva):A S tongue:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom