JF na ccm sikilizeni hili... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JF na ccm sikilizeni hili...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtoboasiri, Apr 20, 2012.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  ...sijashangazwa hata kidogo na maamuzi ya makinda (iwe anaruhusiwa kisheria au la). Najua jambo moja: ccm imeharakishiwa kifo chake. Jana kulikuwa na vikao kati ya mkuu wa mkoa wa Arusha na wamiliki wa Dolly Estate na wakazi wa Arumeru separately. Kwa wale wasio na taarifa, hili ndilo shamba ambalo tumeambiwa hapa ukumbini kuwa kumekuwa na vurugu kati ya wananchi na huyo anaejiita (na ccm wanakubaliana nae katika hilo) kuwa ni mwekezaji. Pamoja na yote yaliyoongelewa, mzee mmoja (na hajui kusoma wala kuandika ila ndie aliepewa jukumu la kuwawakilisha wananchi alisema hivi: "wewe si ndie mkuu wa mkoa? Basi tunakuambia hivi ondoka na huyu Jerome wako vinginevyo damu itamwagika.Anasema wake zetu tu ndio wanaruhusiwa kuingia shambani kwake kuanzia saa sita hadi saa kumi na mbili, anataka kufanya nini nao? Hii ardhi ni yetu"

  Mnategemea perception ya wananchi kuhusu makinda kuzuia juhudi za Mh Zitto kudhibiti wizi serikalini itakuwa nini? Hata kama angeruhusu pinda kupigiwa kura ya kutokuwa na imani siamini kuwa wabunge wa ccm wangebariki pinda kutolewa. Ila kwa kufanya walichofanya wametusaidia kuwaeleza wananchi ambao hadi leo hawajaamka ukweli. Bravo Zitto, mission accomplished! Kilichobaki ni viongozi wa CHADEMA ku-capitalize on this.
   
Loading...