JF inastahili kuchangiwa na wana-JF wote! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JF inastahili kuchangiwa na wana-JF wote!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mchekechoni, Jan 9, 2011.

 1. M

  Mchekechoni JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi binafsi kuanzia January 2011, nitachangia JF kiasi cha Tshs.10,000/= kila mwezi na sina haja ya kukumbushwa bali kwa uaminifu na uadilifu mkubwa nitahakikisha mchango wangu unafika kwa mlengwa (JF) kila ifikapo tarehe 28 ya kila mwezi. Mungu ibariki JF, Mungu ibariki Tanzania, uwape wana-JF wote hekima na moyo wa kuipigania nchi yetu, utuepushe na balaa zote, mikosi na nuksi za kila aina, utupe nguvu ya kustahimiliana na kuvumiliana wakati wa kuchangia hoja bila ya kutukanana, na uwajalie wingi wa heri na afya njema wasimamizi na waendeshaji wote wa forum tukufu ya JF bila kuwasahau waanzilishi na wote walioibeba kwa hali na mali. Wenye jicho la husuda dhidi ya JF, ee Mola wetu ukapambane nao ili JF isonge mbele hata kama umeme utakatika siku saba nchi nzima JF ibaki hewani kutujuza yote yanayojiri juu ya mustakabali wa Taifa letu daima, ee Mola utujalie. Wote tuseme Amina!
   
Loading...