JF ni Jamii Forum. Ni Jukwaa la Jamii.
Mada za siasa, uchumi, kijamii na kisayansi zimenijenga kifikra.
Jamii Forum ni kisima Cha fikra. Imenijenga kifikra na kimawazo.
Nimeifahamu Jamii Forum mwaka 2010 wakati ninakaribia kujiunga chuo, na ni wakati ule siasa zimepamba moto JK anatafuta muhula wa pili.
Kimsingi, purukushani za kisiasa za akina Makamba Yusuf, Nappe na wengineo walinifanya kutafuta maarifa zaidi na niliyapata Jamii Forum maana katika mijadala ile, hao wanasiasa waliihusisha Jamii Forum kwamba Kuna watu wanatoa Siri za chama JamiiForum, kwa hiyo pia nikawa na kiu kujua Jamii Forum Ni kitu gani.
Humu nilikutana na watu wenye weledi kifikra Kama vile
Kiranga,
king kong,
miss chaga, @lara1,
The bold,
Nifah,
Everlyn salt,
Kongosho,
Ben Saanane (RIP), @nappe nnauye,
Mshana Jr ASHA dii na wengineo ambao walichambua mambo kwa kina na kuifanya Jamii Forum iheshimike hapa Tanzania na hata nje ya mipaka.
Pongezi kwenu @jamiiforum,
Mhariri, na haswa Mello, M kwa kazi nzuri ya kukutanisha Watanzania katika jukwaa moja la mijadala huru.
Kazi kubwa iliyopo Sasa ni kuilinda heshima ya Jamii Forum japo irudi ilipokuwa mwaka 2013 maana humu wachangiaji wenye ueledi na staha wanapungua sana.