JF Hip-hop frestyle battle

After short hollday let me fu** the hole
Its not stlye but also hardcore
You make me feel good at time when i score
Need you all the time in my show
Tired for this shit call me if you need some more
 
Ngoma leo day ya mass uzi umepoa moto,

Makuzi upuuzi umezidi hadhi tulipokaribisha watoto,

High class tukasepa kando hapa tukawaacha locals,

Nimerudi humu rivas nimekuja kutema moto,

Washkaji mistari shit na komedi kali za Mboto,

Nakufurahisha na lyrics nakutemea shit sweet,

Kazi na mikazo yangu ni yeye kanibariki,

Uwezo wa mia mia huu uzi nilimiliki,

Nimerudi kama kawa naendeleza muziki.
 
Hiyo ilikua intro imesound good ngoja nitupe mawe,

Nimefika mtu mzima watoto usiku mkalale,

Sikilizia lyrics vina navirusha sadakalawe,

Mjinga okota lyrics ule kozi ya mistari,

Erevuka battle na mimi ukishakua tayari,

Everyday ni boxing day napigana na maisha,

Fu.ck it comes strong inaelekea kunimaliza,

Surviving daily hii nayo ni miujiza, kababaye ka mazingaombwe nig.ga,

Tisha kama njaa omba jesus arudi kabla sijafika,

Mistari finyu na stimu zako za wida,
Unataka battle mkali nimeitika barida
 


oyo unabonga sana,

una kipi cha maana,

mtoto wa jana,

jifunze kupanga vina,

fasihi ni sanaa,

matusi tunakataa,

hata tukiwa baa,

bado beti zinakaa,

sikia broo leo yesu kazaliwa

japo club wengine wanabambiwa

usilewe sana vicoba unadaiwa

kazi na dawa, usije ukavimbiwa
 
Cha maana sina ila nna bonge la mashine,

Linasaga mpaka kokoto mashine langu usipime,

Mwana umeshiba pilau halafu unakanyaga moto,

Nitakupa mistari ucheue ujute kuniquote mkali,

Hater kula mistari mitamu kama asali,

Ukivimbiwa lala ukue, usugue tumbo mpaka ukenue,

Kwa kufatisha hivi vina mpaka washamba mnijue,

Nakufilisi utachalala utamzidi mpaka Eboue,

Dogo usipaniki usiflow maruwe ruwe
 
Bro mi ni noma
Kwa Mitindo huru /

vina vyangu homa
Uliza uchagan hadi mbulu/

Wana wananisoma
Usijilengeshe mi siogopi kukufuru /

Ok nikuweke kwenye list?
Bro we bdo sana kwa mashairi .....
Jipange usikariri ....

Vina vyako havijajipanga
Vivyeupe ka Toto za kimanga

Usitutishe kukufuru ....s n balaa zaid ya gulu

Machiz s miujiza mpka mwanga unaomba kiza ......

S ndo washind tusoshindika .....madokta zaidi ya shika .....
 
Msela umeandika nini mbona umeandika utumbo,

Umejipanga umeshusha shit wana tunashusha nondo,

Umeruka ruka umezama msitu wa vina,

Jichanganye uniquote mkali habari sina,

nakumaliza nakutoa show umethubutu kupima
 
Castr unayumba mwana,
Benny unatoa mistari laini sana,
Kidume nimekuja kuwachana,
Nasimama, nyie mmeinama.

Nani wa kuniweza mimi?,
Rhymes ndo zinaniweka town,
Katu, hakuna wa kunishusha chini,
Acha porojo leta MIC kama huamini.

Kuleni pilau mkishiba mkalale,
Hatutaki jau ku-battle na watoto wa shule,
Msijisahau, kumbukeni kufua sare,
Msilete dharau, chief niko mbele.

Mnatuboa kwa mistari ya visingeli,
Nawapa dawa ya wa kuwaponya akili,
Naona mnaugua mbele ya daktari,
Hampo sawa, hip-hop mshafeli
 
Uko safi bro
Naona unaziweza flow
Ila kwangu uta-blow
Hupati hata droo...

Kwanza, C&P ya ROMA
Wana kitambo tushakusoma
Usipende kitonga kaza mwana
Umiza kichwa, hamna namna

Ati unajikuta mkongwe
Au hujui kuna ngome kongwe
Ipo kitambo kabla ya Kingunge
Historia ipo, unaipata hata kwa mange
 
Tatizo hizi freestyles zipo kavu kavu, hazina beats.
Yaani michano ya kusoma kwa maandishi hata hainogi. Sipati ile feeling.

Wakuu Hii comment yangu sio Freestyle.
 
Dogo una mistari laini dizaini ya super loaf,

Umenitaja legend kama muvi na mkali lufufu,

Nimelala naamshwa eti we ndo unaleta usumbufu,

Jipange tena rudi skuli dogo ukapate cheti,

Sishikiki mi mkali we ngoja mida ya kubeti,
 
Dogo una mistari laini dizaini ya super loaf,

Umenitaja legend kama muvi na mkali lufufu,

Nimelala naamshwa eti we ndo unaleta usumbufu,

Jipange tena rudi skuli dogo ukapate cheti,

Sishikiki mi mkali we ngoja mida ya kubeti,
Ha ha haaaaa nacheka nina amani,
Swala kaingia na simba vitani,
Kujiita legendary ni kufuru, si utani,
Kacheze na watoto, wazee tuko sebuleni.

Nishakuchora, nkakusoma, huna kitu,
Kwenye ubora, nikikoroma, hakai mtu,
Nimetia fora, kila kona, mistari kuntu,
Niko imara, tasimama, we like tu.
 
Dogo umejikaza umeamua kuushika moto,

Mistari haina swaga umeamua kuijaza ukoko,

Time nakimbiza kijiji mwana nachana uzi mzima,

Wote nililamba vyombo hakuna aliyeachwa mzima,

Nashusha kipigo heavy hapa umeachwa mataa,

Napiga lyrics kazi hapa umelivaa balaa
 
Nikisema pipozzz, mtaitika power,

Nina mistari konzi, tega upara upate dawa,

Natoa dozi, kila mtu anapagawa,

Nishakutia simanzi, umebaki unachachawa,

Huna pozi, ka teja mtumia madawa,

Ukubwa wa skonzi, unamezwa na chai ama kahawa,

Kaimbe mapenzi, hip hop tuachie tunaojua,
 

Unafosi nitege kipara chunga usipate mimba,

Kama Joh makinikiona kibinda nadinda,

Simanzi umtie nani na swaga zako za Mpoto,

Tunafreestyle unaghani na vina vyako goloko,

Naiburuza hii area wenzako walitoka nduki,

Haunigusi hauniwezi hapa juu haunishushi,

We ni bado sana kwenye freestyle mamluki,

Mapenzi hatuimbi tunafanya we bikra huwezi jua,

Niquote tena mama niendelee kukamua
 
Dogo ntakusugua ukizidiwa nipe like,

Hua nakua beast kila nnaposhika maiki,

Hamna wa kunizuia hii ngoma siyo simpo,

Sisimami popote I do this for ma people,

Mistari imekushika mkwiji mzembe unachechemea,

Umebip ukadhani sipigi unashindwa kuendelea,

Leo niko na mood nakuzima ka moto na kifaru,

Usione wenzako wajinga wakiniona wanatoka baru
 


Pedophile bars, bro you can’t bruise/

Get slide on madmass, nigga you can't cruise/

Rock depth, I’m the best, This has no contest/

Even without crosses, I'm blessed like a funfest/

Eti freestyle king!, selling birds but they ain’t got no wings?/

Balling like brown kingpin, mistari imekupata unatoka jasho Jing/
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…