Jeska Kishoa acha kutuhadaa Wananchi wa Iramba Magharibi

Jeska Kishoa acha kutuhadaa Wananchi wa Iramba Magharibi

KANDA MBILI

Member
Joined
Jul 9, 2012
Posts
60
Reaction score
57
Ni lini wapinzani tutakuwa mbadala wa chama tawala kama sisi wenyewe tunaendelea kujitafuna. Jana tumeona majimbo mengi CCM wakipita bila kupingwa kutokana na makosa tunayoyafanya wenyewe na kuwapa nafasi hawa wakoloni weusi kuzidi kututawala.

Dada yangu Jeska wewe siyo mtu wa kufanya makosa kama haya una uzoefu na siasa za upinzani na umekuwa mbunge kwa kipindi cha miaka 5 ukiwa upinzani.

Nani asiyejua kuwa Mwigulu kashamalizana na wewe mnabaki kutudanganya sisi kwamba mnaonewa kumbe ulishapewa chako. Naamini hiyo uliyopewa na Mwigulu pamoja na pension yako ya ubunge vitakusaidia kwenye maisha yako.

Tunaoumia ni sisi wapinzani ambao tunahangaika mchana na usiku kutafuta ushindi lakini nyie mnakuja kutumalizia mezani kwa tamaa zenu na kutanguliza maslahi yenu mbele.

Ni nani asiyemjua Mwigulu kwa siasa zake chafu hadi anadiliki kujiita Mamba. Mimi ni mtu pekee ambaye nilipingana na kamati kumpitisha Jeska kupambana na Mwigulu maana nilijua ni sawa na kuwakabidhi jimbo CCM asubuhi na mapema. Ilibidi tujifunze kwa Prof Kitila ambaye alijiandaa zaidi ya miaka mitatu kumtoa Mwigulu lakini aliondoka jua linawaka kabla jua halichamoza kutokana na rafu za Mwigulu.

Leo hii Jeska mnamkabidhi kijiti ambaye ni mke wa CCM mna uhakika ana ajenda ya dhati ya kukichukia chama tawala. Mimi ninavyochukia CCM hata mke wangu akiwa huko naachana naye leo hii mtu ambaye mume wake kashahamia CCM eti ndio mnampa nafasi ya kwenda kukomboa jimbo.

Sasa hivi Jeska anajilalamisha kwenye mitandao kuwa Mwigulu anamfanyia hujuma wakati ni yeye na tamaa zake. Ilibidi tujifunze 2015 Mwigulu hakufanya kampeni alikuja siku mbili na bado akachukua jimbo tena tunamuamini huyo huyo eti sasa amekuwa muarobaini wa kuondoa mpinzani. Hii ni kuwachekesha watu ambao hawataki kucheka. Hili jimbo ni kwamba tumelitoa sadaka kwa mtu ambaye mchana ni mpinzani halafu usiku ni CCM.

Mwigulu huyu huyu ambaye ametumika kutuumiza upinzani ni nani ambaye hajui historia ya uchaguzi wa Igunga nani ambaye hajui uchaguzi wa Kalenga?. Ifike kipindi tujue ukweli tunapotaka kupambana na hawa watawala lazima tujipange sawasawa kuwakabili na tuwatafute watu wenye nia ya dhati ila tusiangalie urembo wao. Sijawahi kumpinga Ester Bulaya wala Halima Mdee ila huyu Jeska Kishoa ni kwamba tumeingia kwenye choo cha kike.

Hivi kweli kabisa Jeska Kishoa ndio wa kuwa na makosa kwenye ujazaji wa fomu ndio ujue kwamba huyo mtu kashapewa chake mapema. Angekuwa mtu mgeni nisingelalamika. Leo hii tunawapa watu majimbo mapema kabla ya kampeni.

Sitahama upinzani ila ipo siku naamini wapinzani tutapata watu sahihi wenye nia ya dhati. Cha muhimu Jeska unanitia kichefu chefu unapojilalamisha mtandaoni wakati unaujua ukweli wako. Basi haya umeishakabidhi mapema jimbo ingia mapema kwenye kumtafutia kura Tundu Lisu ambaye tunaamini ni kusudi la Mungu.

People' s Power
 
Haya majina ya akina Jeska naona yanazidi kushika hatamu kila panapo kucha.
 
Back
Top Bottom