Jeshi letu linatumika vibaya

Naomba nikukumbushe tu mtoa thread, january 9, 2018 Wizara ya kilimo ilitumia gari za jeshi kupeleka Mbolea mkoani Rukwa baada ya Mh Rais kuwawakia Wizara.
huyu hafahamu hata majuku ya Amiri Jeshi Mkuu yupo tu kishabiki tu
 
huyu hafahamu hata majuku ya Amiri Jeshi Mkuu yupo tu kishabiki tuView attachment 930518
Usitumie vibaya vifungu vya kisheria ili kuhalalisha upumbavu wa rais wetu... kwa hiyo kwakuwa na uwezo wa kuamuru majeshi basi ndio kila jambo..?? Kwahiyo hata akitaka agongewe mkewe sawa tu?? Tumia sheria ipasavyo... kwenye ulazima ndio unapaswa kutumia nguvu.. kuna hatari yoyote ya iliyotukabili inayopelekea kutumia majeshi yetu hapo??
 
Nilishangaa kusikia ile kauli kwamba kuna wafanya biashara kariakoo ambao wata chukuliwa hatua na JWTZ...
 
Ila kujenga ukuta Mererani kuzuwia Tanzanite isiibiwe ni sawa. Wala hatukusikia hata siku moja jeshi linatumika vibaya, sijui kwasababu kule ni Arusha?
Kwani Arusha kuna nini? Kwani Jiwe nj mmeru?
 

Kama hafla ya kijeshi huko Arusha ilitumika kupokea madiwani waliohamia ccm ndio itakuwa kubeba korosho?
 

Mkuu ukitaka kujua wafanyabiashara wana fitina, usishangae ikasemekana korosho zetu zina sumu kuvu. Haya mambo hayahitaji nguvu.
 
Mbona mbolea ilipelekwa na jeshi kuna kipindi mahindi yalisafirishwa na jeshi kuna Madaraja mengi yamejengwa na jeshi
 
Kitakachotumika ni kitengo cha usafirishaji ambacho ni jukumu lake pia, JESHI NI MFUMO ULIOKAMILIKA, Madaktari, wajenzi n.k wote wapo, hujawahi ona jeshi lina hospitali?
 
wadau tusilaumu kila wakati hilo ni jukumu mojawapo la jeshi katika kipindi cha amani, primary task ya jeshi ni ulinzi lakini nje ya ulinzi majeshi yetu yanaweza kufanya kazi nyingine za kuisaidia serikali na jamii mfano katika maafa pamoja na majanga mbalimbali kwa hiyo mheshimiwa Rais kuyaagiza majeshi wafanye hiyo kazi kwa mujibu wa maandiko ya Katiba yetu bado yuko sawa kabisa sio kila kitu cha kupinga, kabla hujapinga kitu lazima uje na hoja ya ushawishi yenye kuonesha kwamba hicho unachokipinga ni sahihi au laah, kwa maamuzi ya Mheshimiwa atakuwa amewasaidia sana wakulima.
 
Hata hiyo ni kazi ya jeshi pia mkubwa
 
Account yako imedukuliwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…