beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,881
- 6,378
Jeshi la Sudan limesema Baraza la Kijeshi la nchi hiyo limezima jaribio la mapinduzi. Kwa mujibu wa Jenerali Jamal Omar maafisa 12 na askari wanne wamekamatwa kuhusiana na jaribio hilo.
Omar amewataja maafisa hao kuwa wanatoka jeshini na idara za usalama za nchi, baadhi yao wamestaafu.
Kwenye taarifa yake aliyoitoa kupitia televisheni ya taifa, Jenerali Omar amesema tukio hilo ni njama za kukwamisha makubaliano yaliyofikiwa baina ya baraza la kijeshi la mpito na muungano wa uhuru na mabadiliko.
Tangazo hilo lililotolewa usiku wa jana, linakuja mnamo wakati washauri wa kisheria wa baraza hilo na viongozi wa waandamanaji wakijadiliana juu ya makubaliano ya wiki iliyopita juu ya kugawana madaraka, yaliyofanikishwa na Umoja wa Afrika na ujumbe wa Ethiopia.
Intaneti imerejeshwa nchini humo kuanzia siku ya Jumatano.