technically
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 12,485
- 50,898
Hii double standard mnayofanya ni aibu kwa taifa letu!
Niwape tu mfano kwangu nimekaa Uingereza kwa miaka mitatu sasa sijawahi kuombwa kitambulisho na polisi. Yaani wakikuangalia tu hivi washajua wewe ni suspects au innocent.
Unaweza kushangaa wanakuacha wewe mtu mweusi umepita lakini nyuma akaja mzungu wakamsimamisha. Hiyo ni elimu tena.
Wenyewe wameenda mbali zaidi kwenye ulinzi shirikishi wanatumia Facebook, Twitter na Instagram kukamata wahalifu. Huruhusu watu kuwapiga picha au kuchukua video watu wanaotenda makosa hadharani na kuzirusha kwa mitandao hivyo polisi hutumia kama ushahidi.
Kama mnakumbuka pia wale vijana wahuni walioingia mtaani kipindi kile hakuna polisi aliyetumia nguvu kuwaondoa walichofanya waliweka CCTV vizuri zikanasa kila mtu aliyekuwa akifanya uhalifu na baadae walipomaliza wakaanza kukamata mmoja baada ya mwingine.
Sijawahi kuona polisi wakifanya mzaha kama wanavyofanya polisi wetu Tanzania. Polisi hapa ni taasisi na ni mhimili ambao haufungamani na upande wowote.
Kazi zao zimeainishwa kwenye Katiba kuwa;
1 : Kulinda raia na Mali zao..
2 : Kuokoa mali mara yatokeapo majanga kama moto ajali
3 : Kumshauri waziri wa mambo ya ndani kuhusu njia bora za kuwepo usalama.
etc.
Wapo hadi na sheria ukimkamata mtu bila kufanya uchunguzi wa kutosha ukashindwa kesi unamlipa fidia.
Narudi Nyuma, polisi ni taasisi hivi kwanini kila kamanda wa mkoa anaongea mambo yake kuhusu mambo yanayohusu taifa, kwanini mnavuka mipaka yenu ya kazi?
Kazi zenu zinapishana nini na kazi za polisi wengine duniani? Mimi ninavyojua tulipata Uhuru toka kwa Uingereza ndio maana sheria zetu nyingi zinafanana ila jinsi ya kutekeleza hizo sheria ndio tatizo.
Yaani mnakosa hata msemaji Mwenye weledi? Yaani kamanda wa Dodoma anasema hivi wa Mwanza vile wa Dar vile swali linakuja je hakuna wasemaji katika taasisi zenu anayeweza kupewa kazi ya kuongelea mambo yenu?
Mmeshindwa kukamata waalifu mmebaki kukimbizana na watu wasio na athari kwa usalama wa nchi mko tayari kumkamata Lissu. Ila jambazi aliyeua watu msikitini akiwatoroka tena mikononi mwenu? Are you serious kweli?
Wito kwa Serikali chunguzeni pia hizi nyota zao kamanda mzima nyota zaidi ya tatu anasema uongo tena hatharani hana weledi. Shame on you!
Hizi double standard tatizo nini? na Kwanini? Kama ni shinikizo kwanini msijiuzulu? Kama mnatumwa kusema kwanini msimwambie waziwazi aliyewatuma kuwa haiwezekani? Kama ni kulinda ugali kwanini msiende shule kuongeza elimu na kuachana na kuburuzwa na wanaowatumia? Kwanini mnakuwa kama tiara?
Tatizo ni shule. Wanajamvi, mtakubaliana na mimi mtu aliyesoma kwa umakini hawezi kuwa askari Tanzania imebaki kuwa kazi ya kuokota ndo maana mnaburuzwa na kuzungushwa kama tiara kila siku.
Niwapongeze sana JWTZ kwa kuwa weledi kwenye suala la kuitengeneza JWTZ kuwa taasisi imara yenye msemaji mmoja. Ni nadra sana kumsikia afisa wa JWTZ akiongelea mambo madogo yanayotakiwa kusemwa na msemaji. Na hii ni kwa sababu wasomi kiasi wamejipenyeza ndani ya JWTZ sio kama polisi.
Niwakumbushe tu tengenezeni polisi taasisi sio polisi tiara. Igeni mfano wa JWTZ na taasisi zingine duniani kama CIA, FBI, RTI, SIA etc
Asanteee!