Jeshi la polisi mkoani Simiyu lawashikilia watu 3 kwa tuhuma za kuwakata vikongwe mapanga

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Jeshi la polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu watatu wakazi wa kijiji cha Kadoto wilayani Maswa kwa tuhuma za kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake mama mmoja mkazi wa wilayani Maswa na kumsababishia maumivu makali wakimtuhumu kuwa ni mchawi.

Akiongea na waandishi wa habari katika hospitali ya wilaya ya Maswa ambako mama huyo amelazwa akiendelea kupata matibabu,kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu kamishina msaidizi wa polisi Jonathan Shana amesema kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo march 24,mwaka huu majira ya usiku huko katika kijiji cha Kadoto baada ya kukodiwa na mtu mmoja ambaye ni jirani yake na huyo mama jina lake linahifadhiwa aliyekuwa akimtuhumu kuwa amekuwa akiuwa watoto wake.

Amesema baada ya kufanya tukio hilo walitoroka na wasamalia wema waliweza kumchukuwa mama huyo na kumpeleka katika hospitali na kwamba watuhumiwa hao walifanikiwa kutoroka lakini kutokana na jitihada za polisi waliweza kukamatwa.

Hata hivyo watuhumiwa hao baada ya kuhojiwa na ITV wamekiri kuwa wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa kulipwa ujira wa shilingi laki nne.

Katika hatua nyingine jeshi hilo linamshikilia pia bibi mmoja aitwaye Joyce Mganga mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa mtaa wa Sima wilayani Bariadi kwa tuhuma za kuwafanyia ukatili wajukuu zake wawili wa kike kwa kuwachoma moto wakishirikiana na kijana wake ambaye ametoroka.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom