Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linafanya uchunguzi juu ya mauaji ya watu 7 yaliotokea Sengerema

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
1.jpg

Kwamba tarehe 11.05.2016 siku ya jumatano majira ya saa 03:45hrs usiku katika Kijiji na Kata ya Sima Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, watu wawili wasiofahamika majina wakiwa na mapanga walivunja mlango na kuingia kwenye nyumba ya Mama Eugenia Philipo miaka 60, akiwa amelala na familia yake na kuwakata mapanga sehemu mbalimbali za miili yao hadi kufariki papo hapo, Mama mwenye Kaya Bi Eugeni, Mdogo wake, Watoto, pamoja na watu wengine wawili waliokua wakifanya kazi hapo nyumbani kwao wakitokea Ngara Mkoani Kagera.

Waliouawa 1. Eugenia Philipo miaka 60 Mama mwenye Kaya, 2. Maria Philipo miaka 50, mdogo wa Mama Mwenye Kaya 3.Mabula Makeleja miaka 20 mwanafunzi wa kidato cha nne, 4. Mkiwa Philipo mika 12, mwanafunzi shule ya msingi 5. Leonard Aloyce miaka 13 mwanafunzi shule ya msingi sima wote wa familia moja na 6. Donald miaka 40, pamoja na 7. Samson miaka 23 wakazi wa Ngara waliokuwa wakifanyakazi hapo nyumbani kwa Bi Eugeni.

Aidha katika utekelezaji wa mauaji hayo watu hao walianza kuingia kwenye nyumba walipokuwa wamelala watoto wa familia hiyo pamoja na wafanyakazi, na baada ya kuwakata mapanga hadi kuwaua waliingia kwenye nyumba ya jirani alipokuwa amelala Mama mwenye Kaya na mdogo wake Bi Maria na kuwaua vivyo hivyo, kisha wakaondoka eneo la tukio na kwenda kusiko julikana. Huku watoto wengine wanne wakinusurika kwenye mauaji hayo baada ya kujificha chini ya uvungu wa kitanda.

Jeshi la Polisi linawashikilia watu nane kwa mahojiano dhidi ya mauaji hayo na msako mkali wa kuwasaka wahusika wengine waliohusika kwa namna yeyote katika mauaji hayo bado unaendelea.

Chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana, uchunguzi bado unaendelea. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawaomba wananchi wenye mapenzi mema na nchi yao watusaidie kutupa taarifa za wahusika wa mauaji hayo ili tuweze kuwakamata.

Imetolewa na:
SACP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
 
Back
Top Bottom