Jeshi la polisi liruhusu maandamano ya amani kumuunga mkono Rais!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
36,140
29,670
Jeshi la polisi liombwe kuruhusu maandamano ya amani ya watanzania wazalendo bila kujali itikadi ya vyama ili kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais za kupambana na wizi,ubadhirifu,unyonyaji na ukwepaji kodi unaofanywa na baadhi ya wawekezaji wasio waaminifu!

Vijana wa Vyuo vikuu hii ni fursa ya kujitanabaisha kuwa TAIFA liko hai na liko tayari kwa mapambano ya muda mrefu hadi pale Maisha na Ustawi wa Tanzania yatakapoboreka kwa kadri ya Mungu alivyotujalia.
.....

VIVA MAMA TANZANIA!
 
Tuandamane wakati vita havijaisha? Yakitokea ya kutokea tuaibike taifa zima.
 
Tatizo vijana wengi na wanachuo ni watoto wa makaburu, hawatoandamana. Labda maandamo yawe ya kuwaunga mkono acacia au kushika ukuta wangejaa. Wazo zuri ila hata tukimuunga mkono rais kimoyo moyo si mbaya. Hi nchi kuna mabazazi hawapendi maendeleo wanathamini tu matumbo yao. Ikiwa rais anatetea rasilimali mnapinga kwa manufaa ya nani?
 
Akili ndogo waandamane kuomba msamaha wananchi wa nchi hii kwa kupitisha mikataba ya hovyo.
Lakini leo hii nao wanajifanya wanasikitika kwa ndiyoooooo zao.
 
Jeshi la polisi liombwe kuruhusu maandamano ya amani ya watanzania wazalendo bila kujali itikadi ya vyama ili kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais za kupambana na wizi,ubadhirifu,unyonyaji na ukwepaji kodi unaofanywa na baadhi ya wawekezaji wasio waaminifu!

Naunga mkono hoja....Maaandamano hayo yaendane na kuwalaani wale wote waliosaini mikataba ya kuigharimu nchi yetu

Wale wote walioutunga sheria Mbovu na Kusema kwa Nguvu NDIOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
 
Eti 'kijana wa chuo kikuu' huku unanikata 15% na tulikubaliana 8%?
Haya tangulia barabarani nitakukuta.
 
Hili jambo likifanywa kishabiki na kisiasa litaharibu maana na Ku loose support kwa watu kama Mimi. Washauri wabaya kama wewe wakae mbali.
Jeshi la polisi liombwe kuruhusu maandamano ya amani ya watanzania wazalendo bila kujali itikadi ya vyama ili kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais za kupambana na wizi,ubadhirifu,unyonyaji na ukwepaji kodi unaofanywa na baadhi ya wawekezaji wasio waaminifu!

Vijana wa Vyuo vikuu hii ni fursa ya kujitanabaisha kuwa TAIFA liko hai na liko tayari kwa mapambano ya muda mrefu hadi pale Maisha na Ustawi wa Tanzania yatakapoboreka kwa kadri ya Mungu alivyotujalia.
.....

VIVA MAMA TANZANIA!
 
Baada ya hapo liruhusu na maandamano ya kutaka CCM iondoke madakani kwa kushindwa kulinda maliasili za nchi na ikibidi walioko jela nao wote waachiwe.
Hata CCM ikiondoka madarakani ...bila kuwashughulikia hawa wezi bado tutaendelea kuibiwa tu...weka uzalendo mbele kidogo tu hata kwa wiki tu...halafu tutarudi kwenye ushindani wa kisiasa.
 
Hili jambo likifanywa kishabiki na kisiasa litaharibu maana na Ku loose support kwa watu kama Mimi. Washauri wabaya kama wewe wakae mbali.
Mkuu ina maana huoni umuhimu wa demo...katika suala hili?Huamini kwamba tumeibiwa?

Magufuli has done his part...amewasha moto wa mabadiliko ya kweli...na haitakuja kutokea tena defining moment kama hii huko mbeleni.
 
a64a4bad875baaade36c4dd60ab38128.jpg
 
Mimi nitaandamana hata kwa kukabiliana na polisi akiondoa kinga ya rais kushtakiwa.
 
Kwani nani kasema Rais haungwi mkono!? Alafu pia ni Serikali ipi iliyofanya hayo madudu kama sio Serikali ya CCM!? me nadhani tungeanza kwanza kwa kuandamana kudai katika mpya ili Rais Magufuli awe Rais Huru asiye chini ya chama cha siasa baada ya kuiondoa ccm na kuizika milele
 
Mbona report iliyotolewa imeshatoa majibu yaliyojitosheleza; inasema " kampuni kufanya kazi bila kusajiliwa duniani yapo Tanzania TU"

Tunataka maandamano ya kulazimisha serikali iwaombe msamaha Watanzania na kiwango chote cha pesa kilichotajwa kupotea kiwe kimerejeshwa hazina mapema iwezekanavyo kabla ya 01/01/2018
 
Back
Top Bottom