Jeshi la Polisi linavyowarudisha wananchi kwenye umasikini

Malilambwiga

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
485
296
Serikali iliruhusu kwa mujibu wa sheria pikipiki za magurudumu mawili maarufu kama bodaboda na magurudumu matatu maarufu kama bajaji kubeba abiria.

Uamuzi huu wa serikali ulifanywa kwa lengo la kupambana na uhaba wa ajira hususani kwa vijana hivyo kuwawezesha kujikimu.

Kama tunavyofahamu kila fulsa inapopatikana hukabiliwa pia na changamoto zake. Tatizo ambalo limekuwa likiikabili sekita hii ya bodaboda na bajaji ni kukamatwa kwa pikipiki hizo na kukaa katika vituo vya Polisi kwa muda mrefu bila kutolewa uamuzi aidha wa kurudishwa mikononi mwa wamiliki au vinginevyo.

Ukiachilia mbali bodaboda/bajaji zilizokamatwa kwa kuibiwa au kuhusika ktk uhalifu, sehemu kubwa ni zile zilizopata ajali au kushindwa kulipa faini kwa wahusika hivyo kupelekea kukaa vituoni kwa muda mrefu na kati yake zikifikia hatua ya kuoza na kuwa chuma chakavu.

Hili ni eneo mojawapo ambalo Jeshi la Polisi limeshindwa kuwa na maamuzi sahihi na kwa wakati hivyo kuwarudisha kwenye lindi la umasikini wananchi waliokuwa wameamua kujikwamua kiuchumi kupitia pikipiki na bajaji.

Kunahitajika mageuzi makubwa ndani ya Jeshi la Polisi na katika mfumo wa mahakama zetu namna bora ya kushughulikia vielelezo kwa muda mfupi.

Inauma pindi pikipiki yako inapoibiwa kisha ikakamatwa na kuozea kituo cha Polisi badala ya kumnufaisha mwenyewe.

Kwa sasa hivi kila kituo kikubwa cha Polisi utachokwenda utakuta lundo kubwa la pikipiki zikiendelea kuoza bila maamuzi.

Nimeshindwa kuweka picha sheria hairuhusu kupiga picha maeneo ya kijeshi.
 
Back
Top Bottom