cantonna
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 1,120
- 439
BY, ZITTO KABWE;
Jeshi la Polisi wametoa kauli kufafanua uzuiwaji wa mikutano ya hadhara ya vyama vya Siasa.
Polisi wanasema kuwa ' WAMEZUIA' mikutano ya hadhara na sio mikutano ya KIKATIBA ya Vyama vya Siasa.
Hata hivyo Kamishna wa Polisi Nsato Mssanzya hakunukuu kifungu chochote cha Katiba kinachompa yeye au jeshi la Polisi mamlaka ya kuruhusu au kutoruhusu mikutano ya vyama.
Pia Polisi sio mamlaka ya kutafsiri Sheria ya Vyama vya Siasa na kujua Vikao vya kikatiba ni vipi.
Polisi wametoa ufafanuzi wao kwa sababu ya Mkutano Mkuu wa CCM. Wanasahau kuwa mkutano waliozuia wa Act Wazalendo Kongamano la Bajeti ni kwa mujibu taratibu za Chama chetu kupitia Mfumo wa kuendesha Chama kupitia Kamati za Kitaifa.
Kongamano lilikuwa ni shughuli ya kitendaji ya Kamati ya Fedha na Miradi ya ACT Wazalendo.
Pia naamini kuwa mahafali ya CHASO ni sehemu ya kanuni za Chama chao. Ufafanuzi wa Polisi unaonyesha dhahiri kuwa Jeshi hilo linaipendelea CCM.
Tutaona maajabu zaidi baada ya Mkutano Mkuu wa CCM. Chama hicho kina utaratibu wa kuzungusha Viongozi wao wapya kwenye miji mikubwa.
Magufuli anaenda kuwa anointed kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Chama ambacho yeye hajawahi kuwa hata Balozi wa Shina.
CCM wataacha utaratibu wao wa miaka yote kutambulisha Viongozi wao? Polisi watakuja tena na ufafanuzi mwingine? Tusubiri tuone. Somo?
Viongozi wajifunze kufikiri kabla ya kutamka. Matamko ya MwendoKasi haya yataleta madhara makubwa kwa Nchi.