Jeshi la polisi Kigoma linamshikilia Mganga wa zahanati kwa tuhuma za kubaka mgonjwa

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linamshikilia Mganga wa Zahanati ya kijiji cha Kidahwe wilayani Kigoma kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa aliyekuwa akimtibu katika zahanati ya kijiji hicho.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ferdinand Mtui amemtaja mganga huyo kuwa ni Ibrahim Bundala (29)na kwamba anatuhumiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 14 aliyefika katika zahanati hiyo kwa ajili ya kupata matibabu.

Amesema mtuhumiwa huyo ambaye atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika alitenda kosa hilo baada ya binti huyo kuingia katika chumba cha daktari kwa ajili ya kumueleza ugonjwa anaoumwa.

Katika tukio jingine wahamiaji 55 toka Burundi wamekamatwa katika maeneo mbalimbali baada ya kuingia nchini kinyume cha sheria na wamekabidhiwa idara ya uhamiaji kwa ajili ya taratibu nyingine ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.
 
Itakuwa alitaka kufuata ile kanuni ya madaktari wa wanyama maana wao mgonjwa wao kama hana ugonjwa wenye madhara kwa binadamu na hali yake ni mbaya basi anatoa ruhusa achinjwe na aliwe, kumbe kwa madaktari wa binadamu huruhusiwi kula mgonjwa wako
 
Kuna taarifa za ndani zinadai huyo binti hakubakwa na Mganga, ni mjanja flan alitoka hapo hospitali akiwa salama akapitia kwa mchepuko ndiko alikozinduliwa...alipofika home kwao kwa kuchelewa wakambana ikaonekana alikuwa hospital,ni njama flan kumchafua yule Mganga mtajwa
 
Kuna taarifa za ndani zinadai huyo binti hakubakwa na Mganga, ni mjanja flan alitoka hapo hospitali akiwa salama akapitia kwa mchepuko ndiko alikozinduliwa...alipofika home kwao kwa kuchelewa wakambana ikaonekana alikuwa hospital,ni njama flan kumchafua yule Mganga mtajwa
Kama ni kweli hiyo binti ni Gaidi
 
Back
Top Bottom