Jeshi la Polisi Dar limekamata marobota 10 ya vitenge na pampers, mmiliki alikuwa anakwepa ushuru

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
JESHI la Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekamata Marobota 10 ya vitenge na Katoni 17 za Pampers pamoja na Gari lililotumika kubebea hitu hivyo katika eneo ya Gezaulole lililopo pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya Hindi.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa kukamatwa kwa gari lenye vitu hivyo ni mara baada ya kupewa taarifa na Raia wema kwa kuwa katika eneo hilo kunapitishiwa mali zisizotolewa ushuru.

Siro amesema kuwa Gari lililo kamatwa na Vitenge na Pampers ni aina ya Suzuki Carry lenye namba za usajili T490 CQB ambalo nalo linashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam.

Pia Sirro amesema kuwa mwananchi anaeona kuwa alitelekeza gari hilo lililo na vitu hivyo ajisalimishe Polisi ili apelekwe Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) akalipie ushuru wa vitu hivyo.

Katika Operesheni nyingine Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lilifanikiwa kukamata gari moja la wizi aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 314 DFH ambapo kabla ya kuibwa lilikuwa na namba za usajili T 622 DDR ikiwa gari hilo ni Mali ya Hellen Michael liliibwa maeneo ya Kitunda Kivule ambapo lililuwa limeegeshwa nyumbani kwake. Pia Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam limkamata watu wawili wakiwa na Pikipiki mbili zenye namba za usajili MC343 ASL aina ya Boxer na MC 606 ex aina ya Fercon ambazo ni za wizi na watuhumiwa hao kukuli kuwa wameziiba Pikipiki hizo.

Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam kwa kipindi cha wiki moja limefanikiwa kukamata Pikipiki 519 katika Operesheni ya ukamataji wa Pikipiki kwa makosa mbalimbali operesheni hiyo ilifanywa katika mikoa ya Ilala piki[iki 183,Kinondoni pikipiki 139 na Temeke pikipiki 197.
 
Marobota 10 ya vitenge na katoni 17 za pempas thamani yake haifiki hata 200,000 afu RPC mzima unaita waandishi kuwatangazia..upuuzi mtupu..Hebu atuambie wamekamata majambazi wangapi watoa roho katika kipindi cha wiki moja
 
Unajua maana ya robota kwanza?
unajua bei ya kitenge kimoja?
unajua bei ya katoni 17 ya pampas?

ukishamaliza kunijibu haya maswali matatu ndio nitajua jina ninalotaka kukuita ni makosa au ni sahihi
 
Hahahahahaha
 
Enzi za mzee wa izet emud ma polizia walikuwa wanahongwa nje nje kule geza na escort wanapewa, naona siku izi ma polizia ya mzee Magu yameokoka.
 
Ukanda huu wa mbezi beach, Kawe, mikocheni, kunduchi, msasani,tegeta, bunju, bagamoyo, lindi, mtwara na Tanga ni sehemu ambazo zinaoongoza kwa kupitisha magendo kwa kutumia Majahazi mizigo inatoka Zanzibar na mengine wanashusha bila kulipa kodi nadhani TRA na Jeshi la Polisi wangekuwa makini wangepata Ushuru mwingi na kwenye mpaka mkubwa wa Bahari ya Indi Kuna watu kutoka China, Arabic people na Indian people wanavua sana samaki ktk upande wa Tanzania na wanashusha mizigo isiyolipiwa kodi kwa izi Boti za kibongo za uvuvi
 
Wamedai dau kubwa wamekosana Na Tajiri, huwa wakawakamata wakwepa ushuru hawa Askari wanapatana Kama wao Ndio wafanyabiashara.
 
Ukanda huu wa mbezi beach, Kawe, mikocheni, kunduchi, msasani,tegeta, bunju, bagamoyo, lindi, mtwara na Tanga ni sehemu ambazo zinaoongoza kwa kupitisha magendo kwa kutumia Majahazi mizigo inatoka Zanzibar na mengine wanashusha bila kulipa kodi nadhani TRA na Jeshi la Polisi wangekuwa makini wangepata Ushuru mwingi na kwenye mpaka mkubwa wa Bahari ya Indi Kuna watu kutoka China, Arabic people na Indian people wanavua sana samaki ktk upande wa Tanzania na wanashusha mizigo isiyolipiwa kodi kwa izi Boti za kibongo za uvuvi
Mizigo mingine inatoka kwy meli kubwa ambazo zinakwepa kuja bandarini kulipa kodi
 
Ukanda huu wa mbezi beach, Kawe, mikocheni, kunduchi, msasani,tegeta, bunju, bagamoyo, lindi, mtwara na Tanga ni sehemu ambazo zinaoongoza kwa kupitisha magendo kwa kutumia Majahazi mizigo inatoka Zanzibar na mengine wanashusha bila kulipa kodi nadhani TRA na Jeshi la Polisi wangekuwa makini wangepata Ushuru mwingi na kwenye mpaka mkubwa wa Bahari ya Indi Kuna watu kutoka China, Arabic people na Indian people wanavua sana samaki ktk upande wa Tanzania na wanashusha mizigo isiyolipiwa kodi kwa izi Boti za kibongo za uvuvi

Haya mambo ya ulipaji wa kodi Ni wa hiyari sio Suala la kuviziana, kiuhalisia hawa Tra elimu Yao sijui wanaitumia Wapi? Hawajui Kwanini watu wanakwepa kodi?

Jambo la msingi watasmini tena hizi kodi zao zisizokua hazilipiki. Na wakifanya hivo wanaweza wakikutana Mapato mengi zaidi.
 
Kulipa kodi ni lazima na sio hiari.
 
Marobota 10 ya vitenge na katoni 17 za pempas thamani yake haifiki hata 200,000 afu RPC mzima unaita waandishi kuwatangazia..upuuzi mtupu..Hebu atuambie wamekamata majambazi wangapi watoa roho katika kipindi cha wiki moja
Wewe hebu utufafanulie hapa kulingana na uelewa wako. Robota moja linakuwa na vitenge vingapi na bei zake kabla ya kukurupuka kuwa bei haifiki laki mbili.
 
Haya mambo ya ulipaji wa kodi Ni wa hiyari sio Suala la kuviziana, kiuhalisia hawa Tra elimu Yao sijui wanaitumia Wapi? Hawajui Kwanini watu wanakwepa kodi?

Jambo la msingi watasmini tena hizi kodi zao zisizokua hazilipiki. Na wakifanya hivo wanaweza wakikutana Mapato mengi zaidi.
Mkuu ulipaji kodi ni lazima sio hiyarii na ndo maana kuna sheria anaekwepa kufanya hvyo anapewa adhabu yake
 
Unajua maana ya robota kwanza?
unajua bei ya kitenge kimoja?
unajua bei ya katoni 17 ya pampas?

ukishamaliza kunijibu haya maswali matatu ndio nitajua jina ninalotaka kukuita ni makosa au ni sahihi

Watu kama hao ndio wanaoirudisha nyuma hii nchi, Inamaana ingekua ni yeye ailiowaona hao watu asingetoa taarifa kwa kua vitu vina gharama ndogo,ingawa hata hajui gharama za vitenge.
 
MSIRI WA TRA ASOTEA MGAWO WAKE

❖ Msiri wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambaye alifichua ukwepaji kodi wa Sh7 bilioni, anasotea mgawo wake wa asilimia tatu kwa zaidi ya miezi sita sasa licha ya kodi hiyo kulipwa.

Taarifa Kamili Tumekuwekea Hapa →→→ Msiri wa TRA asotea mgawo wake
 
3de4d03311b6955f21919e2c8709d5fa.jpg
 
Marobota 10 ya vitenge na katoni 17 za pempas thamani yake haifiki hata 200,000 afu RPC mzima unaita waandishi kuwatangazia..upuuzi mtupu..Hebu atuambie wamekamata majambazi wangapi watoa roho katika kipindi cha wiki moja
Umefanana na jina lako ulitaka watu wasipate hiyo habari ili iweje?
 
Back
Top Bottom