ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,417
- 9,603
Jeshi la anga la Marekani(Air force) lasema kwamba linahitaji jumla ya Bombers 165 ili kukabiliana na vitisho toka kwa nchi kama Russia,China,North Korea na Iran.
Pia limeeleza kwamba linahitaji kuongezwa kwa idadi ya ndege mpya(bomber) aina ya B-21 Long Range Strike Bomber ambayo itakua ni stealth hii ni kutokana na kuongezeka kwa mifumo ya kutungulia ndege (surface to air missile)kwa nchi za Russia na China.
Ndege hii mpya ya B-21 Raider kwa sasa ipo kwenye matengenezo chini ya kampuni ya Northrop Grumman watengenezaji wa B-2 stealth bomber.
Ndege hii inaundwa maalumu kwa ajili ya kupenya kwenye maeneo hatari zaidi ambayo yanalindwa na mifumo ya kisasa kama S400,S350V,nk.Pia katika kulinda ndege za washirika na pia drones na vilevile kutumika katika ukusanyaji wa taarifa za kiinteljensia.
Kwa sasa jeshi la anga la Marekani lina jumla ya ndege 159 aina ya bombers ikiwemo 62 B1-B Lancers, 20 -B-2 spirits, na 77 B-52 Stratoforstresses ambayo inatarajiwa kustaafishwa mwaka 2044 ambapo itakua imehudumu kwa miaka 89 tangu mwaka 1955.
Jeshi hilo limesema pia litahitaji jumla ndege 100 aina ya B-21 Raiders, huku ndege moja ikigharimu dola milioni 550 ($550 million; in 2010 dollars) .