Jeshi kwenda Comoro and no to Zanzibar

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,745
Kama iliingiliwa katiba ya Comoro vipi kunashindikana Zanzibar kwa maana Sheni anatawala kimabavu ,kama kuvunja sheria na katiba ndio ameshafanya kama kuiteka tume na kutaka atangazwe kwa kuitisha uchaguzi hewa yeye na genge lake ndio ameshaitisha.

Amiri jeshi Magufuli peleka jeshi kamata Jecha na sheni na genge lao na wafikishe mahakamani walichokifanya kinajulikana kuwa ni uhaini na kwa kuwa hawawezi au Zanzibar hakuwezi kufanyika uhaini basi walichokifanya ni uhuni ,kamata wao na mazombi wao.

Wananchi na vyama ni mambo tofauti ,wananchi wameichagua CUF Zanzibar wapewe haki yao,wahuni waondolewe kwa nguvu za Jeshi la Muungano na ndio moja ya faida za kuwa na chombo cha ulinzi kimuungano , CCM Zanzibar wameleta fyoko fyoko ,shee unangojea niinii au unaogopa vikosi vya SMZ ?
 
Kanal bakari wa comoro alipigwa na majeshi ya tz kwa kung'ang'ania madarakani lakini shein ni ndg yetu hawawezi kuingilia maamzi ya tume.Dah hii imekaa vibaya
 
Mkuu cjaona kaz ya jeshi hapo, labd mahakama walau, istoshe Znz hamna machafuko kama ilivyokuw comoro ss jeshi la kaz gan!!?
 
Mkuu uchaguzi unakaribia tena ni nafasi Kwa wananchi kuonyesha kayamba ni kweli hawakukosea
 
Kuna nini znzbar cha kufanywa na jeshi? Hili ni tatizo la kuacha hisia na mihemko vikutawale badala ya we kuvicontrol
 
Eti tanzania ni nchi ya kidemokrasia, sasa nimeelewa kumbe tunakuwa na demokrasia wakishinda ccm, daaaah inauma saaaana
 
Eti tanzania ni nchi ya kidemokrasia, sasa nimeelewa kumbe tunakuwa na demokrasia wakishinda ccm, daaaah inauma saaaana

Hapo ndipo palipo na tatizo, serikali iliyopo madarakani Zanzibar haipo kisheria ,Jecha hakushirikisha mtu katika matangazo aliyotumwa maana hakuyatangaza kutoka makao yao makuu haijulikani ni wapi alirekodiwa ni kama yule waziri wa Iraq ,demokrasia imepindishwa na watanzania wameshuhudia,

Kama tanzania inaamini inajeshi la Muungano na kazi ni kuzuia fyokofyoko Jecha amesababisha na kuleta mtafaruku ,Magufuli anakimbia kivuli chake lakini asione waZanzibari wamekaa kimya kauli ya kuwa yeye hawezi kuingilia mambo ya Zenji mpaka kuwe na mapambano itakuja kumrudia,wazungu wanaita BACKFIRE ,na Wazenji watatumia mshiko huo huo wa Magufuli ,sasa kama wazenji wanamtega basi ajue mtego unakaribia kunasa.
 
Ndugu yangu umeshaanza viroba siku hizi?? hakukufai huko bakia kwenye togwa tu!
 
Ya togwa na viroba ni wale wenye akili finyu za kufikiri, kilichotendwa Zanzibar kina athari kubwa sana kwa tanzania nzima kama si leo hapo baadae na athari zake ni kwa wale wanao kaa kimya wakiwamo viongozi wa CCM wenye akili timamu na wanaokwenda na wakati ,ona Lowasa,kingunge Sumae ,Nassor Hasani Moyo,Mansour Yusufu Himidi hao ni vigogo waliotoka CCM ,mambo ambayo wakiyaunga mkono leo yanawaangusha vibaya sana.

Sasa wapo wengine ambao hatima yao hawaijui japo ni mawaziri na viongozi wakuu waandamizi ndani ya CCM ila kuna kesho na keshokutwa ,kilichofanywa Zanzibar kitawatia adabu na kwa WaTanzania kwa ujumla.

Siasa kwa wanasiasa ni kazi kama wengine tunaofanya kazi zingine ila kazi zao zina athari kwa wananchi wote na wanayoyafanya ikiwa sio sawa ni lazima yapingwe kwa ujumla wa wananchi bila ya kuegemea mrengo kwamba mimi ni CCM au Chadema au CUF ,waliyoyafanya kina Jecha na Sheni si ya kunyamaziwa au kutumika majeshi kuteka wanaotangaza matokeo sio jambo zuri la kunyamaziwa ni lazima tulipinge.

Sisi kama sisi WaTanzania na sio tuangalie wazungu,wafadhili watutilie mguu na kutuambia hiki sio sawa ,hapa hapakufanyika haki ndio wengine kwa jeuri wakasema tunahitaji kuishi tena katika maisha ya kutawaliwa.

Jeshi limeingilia kati kwa nini ? kumlinda nani ? Kuilinda CCM ? Jeshi kama jeshi halikutenda haki ,kwa nini lisiwe fair ! tena jeshi la Wananchi (JWTZ) ,kama kungekuwa na uvunjivu au viashiria vya amani, basi jeshi lingelinda kituo cha matangazo hadi yamalizwe kutangazwa na sio kuondoka na mtangazaji na kusimamisha matangazo yasiendelee ! Au ingetolewa sababu ya kusimamisha matangazo bila ya wao kuondoka na mtangazaji mkuu ,hili ni tatizo kwa nchi nzima Jeshi limekaa kimya kwani halina cha kuwaambia wananchi halipo pamoja na wananchi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom