TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,747
JESCA JONATHAN MSAMBATAVANGU.
Unatafuta nini kwa kupinga mabadiliko ya katiba ya ccm.
Tunataka ufahamu kuwa mipango yako yote ya kupinga dhamira nzuri ya chama cha mapinduzi imefahamika,umekuwa mstari wa mbele kupinga mipango yote mizuri inayopendekezwa na chama kuhusu mabadiriko ya katiba ya ccm kwa malengo unayoyajua mwenyewe.
Mipango yako yote inafahamika,vikao vyote unavyofanya kushawishi wajumbe wengine waungane na wewe kwenye mandalizi haya inafahamika,hakika umefika hatua mbaya na haya tunayaita mapinduzi dhidi ya uongozi uliopo madarakani pia ni mapinduzi kwa watanzania na wanaccm wote wapenda mabadiriko.
Unashirikiana na watu waliohama ccm na sasa mnahangaika kutengeneza ccm nyingine ndani ya ccm hatimaye mpate kile ambacho mnakitaka ili kuendelea kunufaika kupitia chama badala ya kukitumikia chama na kuwa watumishi wa watanzania.
Tunafahamu pesa unazolipwa kukivuruga chama kuanzia mkoani kwako na maeneo mengine,lakini kwa kuwa umeshajulikana harakati zako hizi zitakuacha kwenye hali mbaya na kamwe hutavumiliwa na hutafanikiwa fahamu hivyo.
Tunakushauri ukae chini utafakari faida na hasara za haya unayofanya,unataka kupata nini hasa,kwakuwa mipango yako yote imefahamika ni vema ukaachana na harakati hizi ambazo hazina afya wala tija kwa chama,serikali hata watanzania kwa ujumla badala yake zitakuharibia wewe zaidi.
Kama kutumika umetumika sana,sasa huu ni wakati wa kuacha kutumika kwakuwa mwisho wake hautakuwa mzuri kwako kwa kuendelea kutumiwa na mafisadi pamoja na madalali wa siasa.
Huu ni wakati wa kuungana pamoja,kuunga mkono mabadiriko ndani ya chama yenye manufaa kwa watu wote na siyo chama kuwa mali ya mtu flani badala ya chama kuwa mali ya wanachama.