Powder
JF-Expert Member
- Jan 6, 2016
- 4,807
- 6,303
Jerry Muro ni Jembe! Uwepo wake Yanga kama Msemaji wa Club, ulichangamsha mashabiki, uliongeza hamasa ya team, Sisi kama mashabiki wa Yanga we will miss you! Mashabiki wa Simba walikua wanatamani kutapika wakisikia unaongea! Wanatamani hata Ungefungiwa maisha, ukijumlisha na matokeo Mabaya ya Simba mwaka huu, halafu wakasikia unazungumzia safari ya Wakimataifa kwenda Angola, walikua wanashikwa kichefuchefu utadhani wana Ujauzito, Haji Manara alikua anaumwa akisikia unazungumza, alikua anatamani hata akupekeleke Mahakamani, Kila mshabiki wa Simba alikuchukia, japo usoni mngecheka Moyoni chuki yao kwako iliongezeka, hao ni Simba!.......
Kwa Mashabiki wa Yanga ilikua burudani tupu kusikia ukiongea, kwa mashabiki wa Yanga wewe ni Jembe, haukuwa tu Msemaji ila Mtetezi wa Club, ulikua zaidi ya Msemaji wa Club, kwenye Uongozi wako tumejua nani wa Kimataifa na nani wa Mchangani, kupitia kwako tumejua Wazee wa kupanda Ndege ni nani na Wazee wa kupanda PERAMIHO BUS SERVICE ni nani! Awamu hii heshima ya Yanga imeongezeka na kuifanya ionekane ni Team ya Wananchi.
Utendaji wako wa kazi haukuweza kumfurahisha kila mmoja, T' EFUEFU ni mmoja wao, kuruhusu Mashabiki kuingia bure kwa maagizo ya Manji kuliwakera T' EFUEFU, kilichowauma zaidi maneno yako, Katibu mkuu alikutolea lugha chafu on air, haikusikika kwao ila wewe ulivyojibu pia wakajumlisha, ikabidi wayajumlishe mpaka Mashtaka ya Haji Manara, ili mradi wa kutie hatiani!
Fanya kama umepata likizo ya Masomo ya Mwaka 1, baada ya kurudi Wabaya wako watakua wanahesabu siku za kubaki Madarakani, mwezi kama huu mwakani Yanga itakua inakaribia kuchukua Club Bingwa Africa, adhabu yako itaisha wakati sahihi.......Kwa Sisi wana Yanga Jerry Muro wewe ni Jembe!!! Tutaukumbuka uwepo wako.....
Usivunjike moyo kiongozi!!!!