Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 761
- 6,985
Yapo maeneo nchi hii yanafahamika kwa kuwa na watu wanaojitambua na wanaoelewa wanataka nini bila kujali wamesoma au hawajasoma, Meru ni moja ya maeneo hayo.
Historia inaonyesha watu walioupiga Vita ukoloni ni pamoja na wameru, watu waliokwenda kudai Uhuru wao ni pamoja na wameru kupitia kwa Mzee Japhet Crilo, watu waliopambana na kufanikiwa kuwa na misingi ya elimu katika kata zote miaka zaidi ya ishirini iliyopita ni wameru, watu hawa wamezaliwa kwenye vyanzo vya maji na pale palipokosa maji kwa kiasi kikubwa viongozi wao waliopita walijitahidi kupeleka maji.
Kisiasa ni eneo linalosifika kwa kutochagua watu kwa vyama vyao Bali wanachagua kwa hoja. Walimpinga mzee mkapa na timu yake ya kampeni adharani na kumdhalilisha wakidai hawalishwi na wanasiasa wanajitaftia wenyewe.
Walimpinga Lowasa na mkwe wake bila kujali fedha alizokuwa nazo na kumchagua Nassary aliyekuwepo Hana kitu. Ni eneo la mfano linaloonyesha kwa vitendo tafsiri ya Uhuru wa kujiamlia mambo yako mwenyewe.
Kwa kipindi kifupi kilichopita hasa awamu ya Tano imepageuza Meru kuwa sehemu ya kujifunza uongozi na sehemu ya kutumia madaraka vibaya hasa kwa wateule wa Mhe. Rais.
Aliongeza mnyeti akaenda na mbinu za kununua watu kwa lengo la kuwapa ajira na kuwarejesha kwenye nafasi yao, aliwapata madiwani wachache lakini hakuweza kuwapata wapiga kura.
Alipoondoka akapelekwa Muro ambaye hata ndani ya chama tawala hawezi kupewa uongozi, akatumwa kuwaongoza watu wanaojitambua na Sasa amekwama. Alichofauli huyu kijana Ni kuwaweka watu ndani kila siku kwa sababu za kisiasa huku maendeleo yakizidi kujitenga na wananchi.
Nakumbuka clip moja alifika kwenye soko moja kugawa vitambulisho wakinamama wakamgomea na kumzomea lakini hakutaka kujifunza.
Leo baada ya muda mrefu wa kutafuta kick kupita nasikia amevamia kikao Cha madiwani na kukivunjia kisa anataka apange wajumbe wa kikao hicho. Kama mkuu wa wilaya anaweza kuvunja kikao Cha baraza la madiwani kwa sababu za hisia za kushindwa kisiasa unategemea maendeleo yatapangwa na Nani?
Jimbo limekabodhiwa kwa Mbunge ambaye pamoja na kusifika na chama kuwa anafedha nyingi hawezi kufanya mradi wowote kwa fedha zake kwani fedha alizonazo ni fedha za kununulia watu siyo za kufanaya maendeleo.
Kijana muro kwa kutumia mamlaka aliyopewa anadhani anawakomoa madiwani anasau kuwa anawakomoa wapiga kura na kujenga chuki kwa wananchi.
Awali Bashiru Aly alikuwa anasherekea matendo ya viongozi wa chama dhidi ya wananchi na watumishi lakini nadhani kila mtu amemsikia akianza kujidai kukemea viongozi hao, si kwamba anawapenda wananchi Bali amebaini kwamba matendo ya watawala yamejaza chuki kwa wapiga kura na kuwafanya wajione yatima kwenye nchi yao.
Hasa wakina Muro wanapaswa kufahamu kwamba madiwani wamechaguliwa na wananchi hivyo kuwadhibiti wasifanye kazi ni kuwadhibiti wananchi wasieleze kero zao.
Lakini pia nipende kuwaweka wazi Wana Arumeru, Muro yupo hapo alipo si kuwasaidia Bali kuakikisha mnaingia kwenye umaskini waweze kuwatawala.
Mkimwona Muro tambueni siyo rafiki wala ndugu Bali ni kiumbe anayedhoofisha maendeleo yenu kwa kuwagawa kwa lengo la kurahisisha kuwatawala. Angalieni mikoa mingi walipo ccm Kama mtasikia kuna madiwani wanavamiwa na DC, hawavamiwi kwa sababu hawajawa kikwazo kwa watawala na wala hawahoji.
Demokrasia iliyoanzishwa na waki Crilo itadumu milele.