Jeraha la Moyo: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jeraha la Moyo:

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tetra, Oct 13, 2012.

 1. T

  Tetra JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 1,522
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Suala uaminifu limeelekezwa kwa wapenzi ktk ndoa au nje ya ndoa.Wapo watu walio nje ya uhusiana fulani.Wao kila kukicha wanapanga,wanabuni mbinu za kila aina ili ampate mke/mme au mchumba wa fulani.Hadi kufikia kubainika na kuvunja uhusiano wa mtu.Kama mwizi umeingia ktk uhusiano huo na kuiba kitu kisicho mali yako.Na uondokapo unaacha aibu na uchungu ktk moyo wa uliyemdanganya na kumwachia hatia.Huu ni ukatili maana unajeruhi moyo,familia na unaweza kuleta madhara ukibainika.Hebu tujifunze kuheshimu uhusiano wa wenzetu Ni kweli,we ni bingwa wa kukubaliwa,unababaisha wengi,,basi JIHESHIMU ili tupunguze idadi ya wanaotendwa na wanaoangukia kwa wenzi wasio wao.Ndoa nyingi zinakosa amani kwa sababu mtu anaingia ktk ndoa akiwa na majeraha,,usilete Jeraha la moyo kwa watu ambao wana uhusiano.Usiende kutoa ushauri kabla hawajakuomba,,huwezi jua neno lako moja laweza kuharibu uhusiano wa watu.
  Neno langu kwako usiwe chanzo cha Jeraha la moyo,kwani moto unaowasha kumchoma jirani yako hukuunguza zaidi wewe kuliko yeye.
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,681
  Likes Received: 943
  Trophy Points: 280
  Mh, hapo kwenye bold duh.....Sasa kama mimi ninavyoandikaga hekaya zangu humu kisha mtu kwa kiherehere chake akasoma na kuamua kutumia mawazo yangu ya kufikirika kwenye uhusiano wake au ndoa yake halafu ikamponyoka naweza kuwa nimechangia eh.....?
   
 3. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  dah, inaelekea umeumizwa eeh! maana ulivyoandika kwa hisia !! pole
   
 4. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Hekaya zako huwa na mafunzo zaidi, kuna watu huwa wanatoa ushauri hata bila ya kutafakari hao ndo hasa inawahusu.
   
 5. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,581
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Ni Maneno mazito, natumaini tutayafanyia kazi.
   
Loading...