Jengo la Yanga kupigwa mnada kutokana na deni la shilingi ml 300, Mkwasa akiri

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
a05e1e626d9d436e537589f1fc4830f2.jpg
Jengo la Makao Makuu ya Klabu ya Yanga lililoko makutano ya mtaa wa Jangwani na Twiga Kariakoo jijini Dar es salaam, liko hatarini kupigwa mnada kutokana na deni la Sh. milioni 300 ambazo klabu hiyo inadaiwa, imefahamika.

Taarifa zilizopatikana jana jijini zinaeleza kuwa kampuni ya udalali ya Msolopa ndiyo imepewa mamlaka ya kusimamia mnada huo.

Akizungumza na gazeti hili jana jioni, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alithibitisha kuwepo kwa deni hilo na kueleza kuwa uongozi umeanza utaratibu wa kulifanyia kazi suala hilo.

Mkwasa alisema kuwa deni hilo limetokana na malimbikizo ya ada ya jengo la kiwanja kinachomilikiwa na klabu hiyo, lakini wanaamini watalilipa kabla ya mchakato huo wa kunadi jengo hilo la Makao Makuu haujafanyika.

"Ni kweli kesi iko katika mahakama ya Ardhi na tumeshaanza kuifanyia kazi", alisema kwa kifupi Mkwasa, Kocha na Mchezaji wa zamani wa timu hiyo.

Chanzo: Nipashe
 
Tatizo letu kubwa waTanzania hua tunangoja tatizo litokee ndiyo tutafute suluhisho, hua hatujikingi na uwezekano wa hilo tatizo kutokea.

Sasa kitu kama kodi kila muda ukifika unajua kua natakiwa kulipa na unajua nisipolipa nini kitafuatia, lakini unangoja mpaka mambo yafike mahakamani na mnada utangazwe ndiyo unasema unashughulikia.
 
Yanga ina mashabiki zaidi ya milioni kumi nchi nzima, wanafika hata milioni ishirini.
Viongozi wakiweka utaratibu mzuri mashabiki wana moyo sana na team yao,ukipata mashabiki milioni moja tu kila mmoja akachanga shilingi mia tano tu tayari una shilingi milioni mia tano, deni linalipwa na chenji ya soda ya wachezaji inarudi.
Sidhani kama mashabiki wenye uchungu na team yao watakuwa tayari kusimama pembeni kuangalia club inakwenda shimoni wakati wanaweza kufanya jambo,kinachokosekana hapa ni ubunifu,na muhimu zaidi washabiki wahakikishiwe uaminifu mipangilio mizuri, nina hakika wataonesha ushirikiano- jambo hili ni kubwa lakini ni dogo sana wanayanga wakiwa na umoja kwani UMOJA NI NGUVU.
 
Simba na Yanga ina washabiki weng sana tatzo kubwa ni UAMINIFU kama una washabiki milion moja tu inatosha kutengeneza not less than 300m in a month time ila tatzo ni UAMINIFU!!
 
TRA chonde chonde ,Yanga hawana hati halali ya jengo.



• Mzee Juma Mamboleo, kikongwe Wa Zaidi Ya Miaka 80 amedai kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa klabu ya Yanga kisheria. Ameonesha Nyaraka Halali Za Kuimiliki Klabu Ya Yanga Na Jengo La klabu hiyo lililopo mtaa wa Jangwani. Uongozi Yanga umesema Nyaraka Hizo Ni Halali lakini Mzee Huyo Anazimiliki Kimakosa.

0734e3bbc69c2ec81ed55b9015ab8d93.jpg
 
Back
Top Bottom