Jengo la NAO Morogogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jengo la NAO Morogogo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chibingo, Jan 17, 2012.

 1. c

  chibingo Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wana JF.
  Jana Mheshimiwa JK kafungua jengo jipya la NAO mjini Morogoro. Katika maelezo yaliyotolewa na CAG gharama za ujenzi wa jengo hilo ni Tsh 161m, source Nipashe ya leo. Nimefurahi na gharama zake za ujenzi. Iweje majengo ya taasisi zingine yenye hadhi kama jengo hilo yagharimu mabilioni ya Shilingi?  Rais Jakaya Kikwete ameitaka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikal(CAG)kutomuogopa kigogo yeyote katika utendaji wake wa kazi.

  Akizungumza katika ufunguzi wa jengo la ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAO) tawi la Morogoro jana, Rais Kikwete alisema hakuna mkubwa zaidi yake yeye katika nchi hii hivyo hakuna haja ya kuogopa kiongozi yoyote, wakiwemo mawaziri.

  Alisema kuwa katiba ya nchi imeipa mamlaka ya kufanya kazi pasipo kuingiliwa na chombo chochote hivyo iwapo viongozi wa Serikali watabainika kufanya ubadhilifu wa matumizi ya fedha za umma wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.

  “Mimi ndiye mkubwa katika nchi hiii nimeshasema wachukulieni hatua bila kuwaogopa viongozi wote wanaobainika kufanya ubadhilifu katika fedha za umma,na mimi naahidi sitowaingilia fanyeni kazi kwa mujibu wa taratibu za kazi zenu,” alisema Rais Kikwete.

  Alisema serikali inatambua umuhimu wa ofisi ya NAO katika kudhibiti mapato ya Serikali na ndiyo maana kwa kutumia rasilimali chache zilizopo inaiwezesha ofisi hiyo kufanya kazi yake kwa uadilifu na kuwa hivi sasa matunda yameanza kuonekana, ikiwemo kupunguza hati chafu.

  Kikwete alisema kuwa awali hati chafu za matumizia ya fedha za umma katika halmashauri mbalimbali nchini zilikuwa nyingi, lakini kutokana na ofisi hiyo kufanyiwa maboresho, hati chafu hizo zimepungua na kusalia nne katika kipindi cha mwaka 2010/11.

  Alitaja moja ya sababu iliyokuwa ikichangia Halmashauri nyingi kupata hati chafu kuwa ni kuajiri wahasibu wasikuwa na utalaam, hali iliyoilazimu Serikali kuamua akuajiri wahasibu 700 na kuwasambaza katika halmashauri hizo.

  “ Halmashauri zilikuwa hazitaki kuajiri wahasibu wenye ujuzi kwa sababu wanazozijua wenyewe,kwahivyo sisi tukaona tuajiri wenyewe na kuwasambaza katika halmashauri hizo na matunda yake ndiyo haya mnayaona hivi sasa,” alisema.

  Alisema katika kuiwezesha Ofisi ya NAO, Serikali imekuwa ikitenga fedha kila mwaka kusaidia ujenzi wa ofisi zao katika ngazi za mikoa iweze kuondoka katika ofisi za wakaguliwa.

  Awali akitoa taarifa za ujenzi wa jengo hilo lilogharimu zaidi ya Sh. milioni 161 mpaka kukamilika, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG),Ludovic Utouh, alisema ofisi yake inaendelea na mpango wa mkakati wa kujipanua ikiwa pamoja na kuimarisha shughuli za ukaguzi zinazoendana na wakati.

  Alisema mfumo mpya unaotumika kwa sasa ni ukaguzi shirikishi unaojumuisha ukaguzi wa thamani ya fedha iliyotumika katika miradi, mfumo ambao umeiwezesha ofisi hiyo kuwa na mafanikio makubwa.

  Hata hivyo Utouh alisema bado ofisi yake inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa majengo.
   
 2. A

  AbasMzeEgyptian JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 406
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 80
  Pasco atakuwa na majibu ya maswali yako
   
Loading...