Jenga Chama Chako Kipya

long'oi

Senior Member
Joined
Jul 16, 2011
Posts
119
Reaction score
69
Wanabodi:

Ni heshima kubwa kutoka kwangu kuja kwenu.

Ni kuhusu hawa Vijana: Wa Kike na Wa Kiume

Si nia yangu kuwaona kana kwamba hawa vijana wabovu au wasio na akili. Ni nia yangu na ni mapenzi yangu kuona vijana hawa wakifanya mambo kwa faida. Nathibitisha kwamba nimefuatilia sakata zima kuanzia lilipoibuliwa na kukolezwa moto na naibu katibu mkuu 'nimeaga kwetu' na huyu kijana mara nyingi watu humwona kama shupavu eight o'clock. Ni kuhusu DHAMBI YA UASI. Singependa kurudi kwenye historia.

Hawa Vijana wa Kikeni na wa Kiumeni kwa tafsiri ya mila na desturi za kiafrika ni kwamba hawana nidhamu. Kitu ambacho hawajui ni kwamba siasa ni kazi na kwamba ni lazima uwe 'strategic', kujiuliza 'what-if-this fail...then' Kitu ambacho 'Naibu Katibu Mkuu' anacho na hicho nampongeza nacho. Hebu wajifunze kwake. Mwone alivyowakana na ameamua kwenye agenda nyingine kabisa ambazo kwake ni 'strategies'. Wanabodi mnaweza kutembelea latest post ya huyu kijana wa kiume kwenye faceebok wall yake mtaona na kuamini ninachosema.

Mfano mzuri ni kama uachane na mwanamke halafu tena uanze kumtumia meseji za matusi, upite mtaani uanze kubwatuka na kutangaza kwa watu ubaya wa yule mwanamke wakati yeye yupo kwa wazazi wake na hakujibu anaendelea. Kisaikolojia "unasafa internal pain'' kuliko yule mwanamke uliemfukuza. Nawashauri Vijana wenzangu, OK imetosha tumieni busara jengeni Chama Chenu Kpya japo cha Magamba. Kama vipi anayetambua kosa lake na kulijutia akalikiri na kuomba msamaha husamehewa. Rudini endelezeni mapambano.

Ni maombi yangu kwenu 'Wanabodi' kutumia thread hii kutoa ushauri mzuri kwa hawa vijana kuhusu namna ya kufanya siasa na kuwa na malengo. they should use what they have today for their future.

Kuna mchungaji mmoja alisema kuna watu wanafanya dhambi mpaka shetani anawashangaa. Mimi nasema hawa vijana wanachokifanya sio Makamanda wanawapuuza Magamba wanajiuliza Heeeee!?

Naomba kutoa Hoja.
 
Naibu katibu mkuu kawachuuza hao masalia na sasa wanahaha wako mjini kuomba omba ufadhili wa jinsi ya kuishi!! Wangekuwa na akili wangejifunza jinsi CCJ ilivyomchuuza mbunge wa Kishapu akaingia kichwa kichwa huku wenzie wakina Sitta, Mwakyembe na Nape Vuvuzela wakisepa!! You should learn from experience for it is the best teacher!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…