Jenerali ulimwengu na hatma ya utawala wa mabavu.

Jenerali ulimwengu na hatma ya utawala wa mabavu.

Miwatamu

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2012
Posts
1,450
Reaction score
492
Katika jamii iliyopoteza maadili, udhaifu (ama wa kimwili, kimali au kiuhusiano), huweka hali inayoweza kuzaa uonevu. Jitu la miraba minne linalopita mtaani likiwadunda wenzake wenye maumbo madogo kwa sababu tu linaweza, linafanya uonevu ambao hawa wadogo hawawezi kukabiliana nalo isipokuwa tu kwa kuunganisha nguvu na kutumia maarifa ya hali ya juu ili kulishikisha adabu jitu hilo onevu.
Mtu mzima anayeishi na watoto (wake au wa ndugu yake) na akawa anawanyang’anya na kula chakula chao na anakila yeye kwa sababu tu watoto hawana la kumfanya, anatenda uonevu mkubwa, na watoto wataendelea kuumia hadi atakapotokea mtu mzima atakayeutambua uonevu huo na kuchukua hatua za kuukomesha.
Je, kipi tunachostahili kujifunza kutokana na mfano huu? Tafakali chukua hatua.


Source: Raia mwema No263
 
Back
Top Bottom