OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,679
- 120,361
Majuzi tu, katika mkutano wa hadhara, Rais John Magufuli alikuwa akiwauliza watu “Nitumbue, nisitumbue?” na watu wakamjibu kwa sauti moja “Tumbua!”
Mikutano ya aina hii, na majibizano ya aina hii baina ya mkuu wa nchi na wananchi wake yanaweza kutoa taswira ya mkuu ambaye amefungamana na watu wake kiasi kwamba anafanya yale tu ambayo wananchi wake wanataka ayafanye, na hili litaonekana kama jambo jema.
Lakini pia ni jambo la hatari, nami nitaeleza. Mimi sina tatizo kubwa na watendaji wa umma “kutumbuliwa” ingawa silipendi sana neno hilo. Silipendi kwa sababu ile ile niliyokwisha kuisema, kwamba tatizo linaloikabili nchi hii si majipu, bali ni saratani, na hakuna utaalamu wa kuitumbua saratani.
Tunaweza kuendelea na kelele za “utumbuaji” hadi miaka mitano ikakatika bila kuona matokeo ya kweli kwa sababu tu tulikuwa hatujabaini tatizo ni nini. Sisi tumefanywa tuamini ni majipu kumbe ni tatizo la msingi zaidi.
Mantiki ya kawaida inaniambia kwamba huyo mtuhumiwa atakuwa tayari amekwisha kupachikwa nembo ya “ufisadi’ kutokana na jinsi alivyotangazwa na mkuu kwenye ule mkutano wa hadhara na wananchi wakamwitikia mkuu kwa kusema kwa sauti moja, “Tumbua!”
Hali hii haina tofauti kubwa sana na utawala wa imla wa mkusanyiko wa halaiki. Pamoja na nia njema kabisa, mkuu anaweza kutumia nguvu ya magenge. Daima wanasiasa watakuwa ni wanasiasa, na si watoa haki. Wanachotaka wanasiasa ni kuona kwamba wanakubalika mbele ya halaiki ya watu na kila wafanyacho kinashangiliwa.
Katika hali tuliyo nayo leo hii, na najua kwamba hali hii imegubikwa na uozo tulioachiwa na watawala wetu waliopita, kuna umuhimu mkubwa wa kupambana na uozo huo. Lakini mapambano hayo hayana budi kuwa na utaratibu unaojulikana, utaratibu unaotabirika. Hili ni muhimu sana kiasi kwamba sijui kama linaweza kuwa na maelezo ya kutosha.
Hatuna budi kujenga utamaduni wa kufuata kanuni, taratibu, sheria na katiba, hata kama tunawashughulikia wale tunaodhani ni waovu. Hatuna haki ya kutenda maovu kwa sababu tu eti tunapambana na watu waovu. Kama tuna uhakika kwamba ni waovu, basi itakuwa rahisi kudhihirisha uovu wao.
Kama tumeshindwa kudhihirisha uovu huo, basi hatuna budi kukiri kwamba kesi yetu ni dhaifu kwa sababu ama wapelelezi wetu hawafai ama kesi yenyewe ilijengwa juu ya misingi ya hisia na siyo hali halisi
Tamko la Rais Magufuli kwamba hata hao wanaotetea majipu nao ni majipu pia linatia hofu ya kweli kwamba tumeanza kuserereka.
Namuomba Rais Magufuli aiangalie tena kauli hii tusije tukajikuta katika mashaka makubwa.
Mashaka hayo nayaona kwa njia mbalimbali, lakini mojawapo ni ile ya wateule wa Magufuli watakaopenda kuchukua hatua zitakazomfurahisha bosi wao, hata kama hatua hizo si sahihi.
Si kila mara tutaweza kupata taarifa za watu walioonewa huko wilayani au vijijini kwa sababu tu wameshukiwa kuwa “mafisadi” au watetezi wa “majipu” ambao nao wanageuka kuwa “majipu”.
Katika matatizo makubwa ambayo nchi hii haina budi kukabiliana nayo, mojawapo ni lile la watu kutotaka kutendeana haki bila mizozo isiyokuwa na tija.