Jemedari Lema wewe bado kijana, pambana ukiwa jela Kisongo kwa muda na sisi tupambane jela ya kitaa

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,380
2,000
Anaandika Celina Donald Chacha.
LEMA WEWE BADO KIJANA ,PAMBANA UKIWA JELA KISONGO KWA MUDA NA SISI TUPAMBANE JELA YA KITAA.
NAJUA WATESI WA SAGA YAKO WANA MAUMIVU YA KUTOSHA LEMA LAKINI NAAMINI UNAMJUA MUNGU UKIWA HUKO OMBA SANA LEMA ZIDISHA SANA LEMA KUOMBA NA MAFUNGO IKIBIDI ILI NIJIONEE NIKIWA KITAA KWA MACHO YA NYAMA......nikitua Ar nitakuadithia.....

NIKITAZAMA KILA UINGIAPO NA UTOKAPO KISONGO TO MAHAKAMANI NAPATA UJASIRI NATAMANI MAWAKILI WA SERIKALI WAENDELEE KUKATA RUFAA JUU YA RUFAA ZAO,UKWELI NAFARIJIKA MNO KWA NAMNA YA KIROHO NAJUA UPO MPANGO MUNGU ANAUANDAA KAMANDA LEMA,SIJAONA UMEKATA TAMAA ,UMEENDELEA KUNG'AA KUWAZIDI WALIO JUU.....hili peke yake nimwambie Mungu Asante....

Nakumbuka Mahakama ilitoa dhamana juu yako Lema,Lakini shetani alivyo Mbwa akawafumba macho Wenye Haki,Mawakili wa Serikali wakakata rufaa kupinga Uamuzi huo wa Mahakama wa kutoa dhamana.......

Asivyo na Haya Shetani ameendelea kusimama bado kwenye viunga vya Mahakama kuwateka Wasio na Hofu ya Mungu.... Tazama hata kufikia sehemu Mawakili wa serikali wakaamua Kukata Rufaa tena dhidi ya Uamuzi wa Mahakama wa kusikiliza Rufaa zao Wenyewe!

Lema Jionee michezo hiyo ya Makusudi tuu watu kucheza na Sheria za kukufanya wewe kurudi Kisongo tena,Mh.Lema ndio maana nasema bdo ukingali kijana ni lazima upitie haya ili sisi Pimbi nje tujifunze kupitia Makosa ya hao tunao waamini..,..,.,.. OMBA SANA LEMA UPO MPANGO HAUJAKAMILIKA MUNGU ANAUANDAA..... ....

LEMA PICHA NILIZOZITUMIA HAPA CHINI NDIZO ZINANIPA UJASILI,FARAJA, MATUMAINI KUWA WEWE UNA MUNGU ,NASIO TUU MUNGU! HATA HOFU YA MUNGU IMEKUTAWALA HIVYO ULIPO NI SAHIHI KWA MUDA KWA SASA KULIKO WAKATI MWINGINE WWTE!Japo natamani Wakirudi Wakuje na Rufaa nyingine kupinga ya Jana Isisikilizwe.............

MAHAKAMA Jana ilipata Ulinzi wa kufa mtu Lema,Ulinzi ulioambatana na kunyimwa hata Watu wa kawaida kuingia ndani ya viunga vya Mahakama kinyume kabisa na sheria za kimahama,nikamkumbuka Mh.Lowasa Tar.31/12/2016 alipokuwaja kukutembelea alisema"Watanzania wana Imani Kubwa na Mahakama kuwa ndio SURUHU" nikajiuliza watanzania gani hao nimejikuta nacheka kwa dharau!

LEMA WEWE NI MWIBA
LEMA WEWE NI KIBOKO
LEMA WEWE MWANAUME
LEMA WEWE UNAOMBA
LEMA MUNGU ATAJIBU
LEMA UTATOKA TUU!!¡!!
FB_IMG_1483620522283.jpg
FB_IMG_1483620519663.jpg
 

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,380
2,000
MAHAKAMA Jana ilipata Ulinzi wa kufa mtu Lema,Ulinzi ulioambatana na kunyimwa hata Watu wa kawaida kuingia ndani ya viunga vya Mahakama kinyume kabisa na sheria za kimahakama,nikamkumbuka Mh.Lowasa Tar.31/12/2016 alipokuja kukutembelea alisema"Watanzania wana Imani Kubwa na Mahakama kuwa ndio SULUHU" nikajiuliza watanzania gani hao nimejikuta nacheka kwa dharau!
 

PRODA LTD

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,005
2,000
Lema ni shujaa Mungu azidi kumpa ujasiri na hekima zaidi katika kusimamia unachokiamini hujawahi kurudi nyuma.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom