Jela miaka 60 kwa kukutwa na mguu wa Twiga

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,717
55,819
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, imewahukumu kifungo cha jumla ya miaka 60 jela washtakiwa watatu waliotiwa hatiani kwa kukutwa na mguu wa twiga kinyume cha sheria za wanyama pori.

Hukumu hiyo imetolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Teotimus Swai, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.


Awali, mwendesha mashtaka Wakili wa Serikali, Jamila Miraji, alisema mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walikamatwa Oktoba 11, mwaka jana saa 5:30 wakiwa na mguu wa twiga kinyume cha sheria za wanyama pori.

Aliieleza mahakama hiyo kwamba washtakiwa walikamatwa na askari wa Tanapa waliokuwa katika doria ndani ya hifadhi ya wanyamapori ya Katavi, ambako waliwakuta na mguu huo wa twiga.

Akitoa hukumu hiyo, hakimu Swai alisema ushahidi uliotolewa mahakamani na upande mashtaka umewatia hatiani watuhumiwa hao.

Kabla ya hukumu hiyo, hakimu Swai alitoa nafasi ya kujitetea kwa watuhumiwa, ambao waliiomba mahakama isitoe adhabu kali kwao kwa kuwa ni wategemezi, maombi ambayo yalitupiliwa mbali.

Waliohukumiwa kwenda jela ni Juma Kinanda (66), Saidi Shabani (42) wote wakazi wa Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora na Rashidi Miraji (64) mkazi wa Inyonga wilayani Mlele.

Chanzo: Mtanzania
 
Uwazi unazidi kuongezeka katika Taasisi za serikali. Hii itasaidia sana katika ukuaji wa nchi. Ombi langu kwa serikali yetu, Tunaomba viongozi wengi wa serikalini na wenyewe waingie Jamii Forum hili wapate taarifa nyingi kuliko kuiona kitofauti, maana hii ni zaidi ya vyombo vyote vya habari apa Tanzania na watanzania wote,
Maana Jamii Forum ni jukwaa kubwa la watanzania waliopo Tanzania na njee ya Tanzania
 
Yaani nchi hii inaonekana ukikutwa na kiungo cha mnyama adhabu yake ni Kali kuliko kukutwa na kiungo cha binadamu
makosa ya ujangili na nyara za wanyamapori yamewekwa katika makosa ya uhujumu uchumi ambayo ukitiwa hatiani kifungo cha chini ni miaka 20 au fine au vyote kwa pamoja
 
Tatizo angekuwa MTU mwingine mzungu au mwarabu asingepigwa mvua hiyo.

Angetoa rushwa angekimbia kwao .

Haki itendeke kwa wote.
 
please wataalamu wa sharia they can help here huyu hakimu katumia vifungu gani vya kisheria kutoa hukumu kama hii?,ndio maana nchi yetu inahitaji mchanganuo mkubwa wa kubadili sharia mama ,KATIBA,hukumu kama hii haitoi dhana ya hukumu ambayo ni kumrekebisha mhalifu sio kumkomoa,
 
Sasa hawa wenye miaka 60 ukiwaongezea na hiyo 60 si wanafia huko? Yaani mtu anaanza kuwinda sungura anapandaaa hadi anawinda lijidude kama hilo, Twiga? Bora angekutwa anawapandisha Ndege
 
makosa ya ujangili na nyara za wanyamapori yamewekwa katika makosa ya uhujumu uchumi ambayo ukitiwa hatiani kifungo cha chini ni miaka 20 au fine au vyote kwa pamoja
bora uwafafanulie mkuu maana hawa vijana wa ufipa kila kitu kulalamika tu
 
Back
Top Bottom