Jela miaka 28 kwa kughushi vyeti. Mbona ni kwa wananchi wa kawaida tu?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Jela miaka 28 kwa kughushi cheti cha uuguzi

Imeandikwa na Flora Mwakasala/Imechapishwa katika gazeti la HabariLeo

MUUGUZI Lucia Ilomo (44) amehukumiwa kifungo cha miaka 28 jela katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam baada ya kupatikana na hatia ya kughushi vyeti vya Uuguzi na Ukunga.

Hakimu Mkazi Augustina Mmbando alitoa hukumu hiyo jana baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi watatu wa upande wa Jamhuri pamoja na utetezi wa mshitakiwa.

Akitoa uamuzi huo jana, Hakimu Mmbando alisema upande wa Jamhuri umethibitisha mashitaka manne dhidi ya mshitakiwa na
katika kila shitaka atatumikia kifungo cha miaka saba jela.

Hata hivyo, alisema Lucia ambaye pia anajulikana kwa jina la Veronica Kuyena, atatumikiwa adhabu hizo kwa wakati mmoja hivyo ni sawa na kifungo cha miaka saba jela.

Lucia alikuwa anakabiliwa na mashitaka sita ya kughushi, kuwasilisha vyeti vya kughushi na kujitambulisha kuwa yeye ni mtu mwingine hata hivyo alipatikana na hati ya mashitaka manne.

Ilidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya Februari 2007 na Mei mwaka jana Dar es Salaam, alighushi cheti cha uuguzi chenye namba 18558 na cheti cha ukunga namba 13568 akionesha kuwa vimetolewa kwake kama Lucia Kazohela jambo ambalo si kweli.

Katika mashitaka mengine ilidaiwa kuwa katika tarehe hizo, mshitakiwa alijitambulisha kuwa yeye Lucia Kazohela kwa kuwasilisha vyeti vya uuguzi na Ukunga akidai kuwa ni vya kwake jambo ambalo si kweli.

Aidha ilidaiwa kuwa, aliwasilisha vyeti hivyo kwa Ofisa Rasilimali watu wa Manispaa ya Kinondoni.

Katika utetezi wake, Lucia alidai kuwa alisoma katika Chuo cha Uuguzi cha Mvumi mwaka 1980, jana aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ana mtoto anayemtegemea.
 
Hivi Naniliu akienda jela miaka 5 tu, ATAKUWAJE?

Maana alizoea .... Halafu ghafla .....


Na lile ..... si wajelajela wata......

Yangu JF

Macho namwachia hakimu!


Si walisemaga jela kuna tabia za kisho...

Dawa ndio hii, Apelekwe kule akaupinge usho... akiwa makao makuu ya usho...


Karibu jela Mr Bashi....

Jina lako jipya ni Miss Seya!


aha!!


Fake mie!
 
Huyu RC aliegushi cheti atapandishwa cheo ili kuwakomoa wenye midomo kumbuka hata hicho cheo alipewa kwa ajili ya midomo yenu.
 
Ni Balaaaa yaani.. Jamaaa anabanwa kila kona na sijui atakwepa hivi hii issue kama ina ukweli ndani yake
 
Magufuri akikaa kimya kwenye hili nitajua yooote anayoyafanya na aliyoyafanya ni usani mtupu
 
Back
Top Bottom