DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Emmanuel Mussa (27), mkulima na mkazi wa Kijiji cha Ighombwe, mkoani Singida, amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la tano wa Shule ya Msingi Ighombwe.
Tukio hilo lilitokea Novemba 12, 2023 katika Kata ya Sepuka, Wilaya ya Ikungi. Baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo katika Mahakama ya Mkoa wa Singida kuanzia Juni 22, 2024, hukumu ilitolewa Agosti 22, 2025 na Hakimu Mhe. Lau Nzoa.
Jeshi la Polisi limetoa wito kwa jamii kushirikiana katika kuwalinda watoto na kusisitiza kuwa halitasita kuchukua hatua kali dhidi ya mtu yeyote atakayehatarisha usalama na haki za watoto.