kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,676
MAHAKAMA ya Wilaya ya Lindi, imemuhukumu kifungo cha mwaka mmoja gerezani mkazi wa Manispaa hiyo, Abdallah Mohamedi Munguja (32), baada ya kupatikana na hatia kwa makosa mawili, likiwemo kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha majeraha ya mwili kwa Karimu Mnwela.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu wa Mahakama hiyo, Aluu Nzowa, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka.
Makosa hayo ni kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha majeraha ya mwili wa Karimu Mnwela, pamoja na uharibifu wa mali ya mlalamikaji huyo.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Hakimu Nzowa alimuuliza Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Rabia Ramadhani, kama ana kumbukumbu ya makosa ya zamani kwa mshitakiwa huyo.
Mwendesha mashitaka huyo alisema hakuwa na kumbukumbu yoyote, lakini akaiomba Mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwake na madereva wengine wasiozingatia sheria za matumizi ya barabara.
Hakimu Nzowa alimuhukumu mshitakiwa huyo kulipa faini ya Sh.35,000 kwa kila kosa alilolifanya, na endapo atashindwa itamlazimu aende jela miezi 12.
Awali, ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka Ramadhani kuwa mshitakiwa alifanya makosa hayo Machi 16 mwaka huu saa 3:0 asubuhi, katika kijiji cha Mahumbika, wilaya na mkoa wa Lindi.
Mwendesha Mashitaka huyo aliiambia Mahakama hiyo kuwa siku hiyo ya tukio, mshitakiwa Munguja akiwa anaendesha gari aina ya Tata T.584 CRH aliigonga Costa yenye namba za usajili T 618 CMU mali ya Ayubu Ally.
Rabia aliiambia Mahakama hiyo kuwa kutokana na kuendesha gari hiyo kwa uzembe alisababisha maumivu ya mwili kwa Mnwele na uharibifu wa gari hilo.
Chanzo: NIPASHE