Kama viungo vyako vyote sba vya fahamu vipo makini, uwezi kushangaa mtuhumiwa wa EPA "Jitu" ameshinda zabuni .....hicho ni kitu kidogo sana kwa zabuni za Serikalini ndugu yangu. Wajuzi wa mambo wanasema ni zabuni chache na "uchwara" kama za ununuzi wa vifaa vya ofisi na kufanya usafi maofisi au kupika na kupamba kwenye dhifa za Serikali ndizo zinazotoka kwa "wabongo wenye urai wa kuzaliwa"
Hii "sisitimu" yetu "wa-tz wenye asili ya Mumbai au Uta-pradesh" na wale wanaoishi Canada na Tz kwa wakati mmoja " wameikaba kila kona!...... Hakuna zabuni itakayotolewa na Serikali usikute sura ya "huko" hata akiomba "Mpori Mnyakyusa", yeye atakuwa kivuli tu anatumika, ukichimba zaidi utakuta nyuma yake yupo "Mwenye asili ya huko......!!!" (ndani naeleweka!)
Jitu asilalamikiwe sana, yeye ni mwakilishi tu wa kampuni ya Escot toka " In -dia" ambayo kisheria inatambulika kama "legal body". Aidha, hta kama "Jitu" hasingehusika moja kwa moja kwenye zabuni aidha kwa jina lake au jina la kampuni yake, bado hakuna Mtanzania anayeweza kujua hiyo ya India ni ya nani kama tusivyojua ya Shirika letu la Reli "TRC" kwenda mdudu "TRL"..Kwani Jeetu ni mwenye asili ya wapi??????? au angepata Manji nae ni wa wapi!!!!!! labda tungekuwa "confortable" angepewa "Mzee wetu wa IPP Media" tungejua labda kama sio wa Kibosho basi wa Huru kishimundu.........Oh, vpi kama angepewa "mzee wetu wa Waraka" (anaye endesha sasa standi kuu ya Mabasi - Ubungo Terminal) tungefurahia?????????...
Inawezekana hata hyo ya India ikawa ya familia ya mmoja kati ya wale wenye asili ya huko au pia ikawa ya mmoja kati yetu (nani alijua yule Yuda wa Isikaliot aliyekuwa anakula na kunywa bure mvinyo ambao Wagalatia, Warumi na Wayunani wenye dhambi walikuwa wakimletea Mwalimu (Yesu Kristu)angefikia siku akubali kubadili fikra na kuanza kutafuta "vijiseti!" wakati akiwa "kundini" na akiwa na uhakika wa ufalme wa mungu wa bure kabisa ambao wengi walikuwa wakiutafuta kwa kusali na kulia kila siku???? Huyu YUDA sijui tumfananishe na nani katika Serikali yetu, ambaye ana acha kuambatana na Bwanake (yule aliyemwita kundini) na kwenda kutafuta "dili" za hela tena za kutoa uhai....(anyway).......
Labda kwa mfano unaoonekana, nani alijua mtu aliyepewa dhamana ya kumshauri Mkuu wa Nchi kwenye masuala yote ya kisheria (Chief Legal Advisor) na ambaye alikuwa akila na kunywa mezani kwa mkuu wa nchi muda anaotaka angeweza kuingia kwenye mtego na kishawishi kibaya cha "kupenda sana vijisenti kuliko nafasi yake na nduguze (Watanzania)....??????? ......
Nadhani mnyororo wa watu hawa wenye asili ya huko ambapo mshinda zabuni ametokea kila mtu anaufahamu !. Kwa taarifa za uhakika, tokea Serikali yetu ilipojitoa kufanya biashara, kumekuwa na utitiri wa makampuni hapa nchini ambayo yamefunguliwa na watanzani wenye asili ya .......(huko mnakomanisha) tena nyingine ni za watoto ambao hata miaka kumi na nan hawajafikisha. Kuna kampuni moja maarufu hapa nchini oofsi zake zipo hapo "Barabara ya Marehemu Baba wa Taifa -Mungu" amrehemu!, hiyo kampuni inakaba uchumi wa nchi kila kona kuanzia inalima, inanunua mazao, inatengeneza na kuagiza toka nje baadhi ya zana za kilimo, inasindika na kuuza au kuleta toka nje mazao an vyakula (mpaka tandare ina meza!), inafuga, inatengeza maji, itatoa huduma za benki, inauza daftari na vifaa vingine vya maofisi, ina maduka ya simu za mikononi, inamiliki timu ya soka, ipo kwenye biashara ya siasa kupitia mmoja wa wakurugenzi wake, inauza vipuri (spear parts), ina maduka ya vifaa vya ndani na samani (fenitures) na maduka y kubadilishi fedha, inafanya biashara ya kusafirisha abiria, inaagiza toka nje madawa ya kilimo na mbolea, ........sina shaka itakuwa na saluni na kumb za starehe pia..... Kwa tetesi toka ndani ya ofisi za umma inasemekana hiyo kampuni ndani yake ina kampuni dada "sister companies" zaidi ya Ishirini na hilo ni uhakika kabisa.
Inapotokea zabuni, kampuni hiyo kubwa na yenye jina huhakikisha kila kampuni yake inaomba ili kuhakikisha ushindi wakati wote na pengine unaweza kukuta ni kampuni za mtu mmoja tu zimeomba zabuni (!!!!!!)........Inasemekana kuwa zabuni nyingi ambazo kampuni hiyo na makampuni yaliyo chini yake imehusika sana Serikalini ni zile za sekta ya kilimo na ununuzi wa vifaa vya ofsi ambapo inadaiwa kuwa nyaraka za zabuni (bidding documents) huwa zinatofautiana kidogo sana hususan kwenye jina la mwomba zabuni, bei, jina la mkurugenzi anaye mweka saini kwenye nyaraka husika na stairi ya maandishi (font type/ size). Ila maelezo mengine yote ndani ya zabuni huwa ni sawa sawa kabisa (copy and paste). Aidha, inadaiwa kuwa hata kwenye barua za kulalamikia pale inapotokea jambo ambalo kampuni hiyo na makampuni yaliyo chini yake yatakuwa hajaridhishwa, mwandishi wa barua husika kwenda Serikalini huwa ni mmoja na unaweza kuona tofauti kwenye jina la kampuni na mtia saini tu.
Katika hali hii wanajamii mnategemea nini kwenye zabuni zinazotangazwa Serikalini????????.... TUNAHITAJI MUDA WA KUJIFUNZA KWA YALE TULIYOAMBIWA TUTATEKELEZEWA, TUSIPOYAJUA LOLOTE LAWEZA KUWA JIBU.............