JKT yalaumiwa kuingia mkataba na mtuhumiwa EPA Bw. Jeetu Patel | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JKT yalaumiwa kuingia mkataba na mtuhumiwa EPA Bw. Jeetu Patel

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 16, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Gladness Mboma, Dodoma

  KAMBI ya Upinzania Bungeni, imeshtushwa na kitendo Jeshi la la Kujenga Taifa (JKT) kuingia mkataba na Bw. Jeetu Patel kuingiza matrekta nchini wakati anakabiliwa na kesi ya wizi wa mabilioni ya fedha kutoka Benki Kuu (BoT) kwenye akaunti ya malipo ya nje (EPA) na kesi yake bado inaendelea .

  Kutokana na hali hiyo Kambi ya Upinzani Bungeni imeitaka serikali kuwaeleza
  Watanzania juu ya jeshi kumtumia mtuhumiwa wa wizi wa fedha za walipa kodi kuingia makubaliano ya kibiashara kwa kutumia udhamini wa fedha za walipa kodi.
  Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani –Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Bw.Joseph Selasini aliyasema hayo bungeni wakati alipokuwa akitoa hotuba kuhusu
  Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012.

  "Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi inayoitwa "Public good,rents and business in
  Tanzania" iliyotolewa na Bw. Brian Cooksey iliyotolewa Juni mwaka jana inasema kuwa serikali imetoa udhamini wa sh. Bilioni 40 kwa SUMA-JKT na shirika hili la jeshi likaingia mkataba na Bw. Patel kuingiza matrekta hapa nchini , sasa ni kwa vipi tena jeshi linaingia nae mkataba wa kufanya mabakubaliano na India kwa udhamini wa fedha za walipa kodi,"alihoji.

  Bw. Selasini alisema kuwa taarifa ya Waziri inaonyesha kuwa sh. Bilioni 1.123
  zilitumika kwa ajili ya utoaji wa matrekta hayo bandarini na hadi sasa matrekta hayo yamewekwa Mwenge Dar es Salaam na mengine wameyaona hapo maeneo ya Kisasa Dodoma. "Swali la kujiuliza ni kweli matrekta haya ni mali ya jeshi au kuna Maofisa wa jeshi wanafanyabiashara hiyo kwa kutumia jina la jeshi na kama ni mali ya jeshi Waziri alieleze bunge hili jeshi lilitarajia kupata faida kiasi gani baada ya kufanya hiyo biashara ya kuuza matrekta hayo,"alisema.

  Alisema kuwa kitendo cha jeshi kujiingiza kwenye biashara ambayo siyo jukumu lake kimsingi linawatia mashaka makubwa sana kama kweli jeshi linatumika kufanya biashara na baadhi ya watu.

  "Hoja hii inapata nguvu kutoka kwenye hotuba ya Mheshimiwa waziri wakati
  akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya ulinzi na Jeshi la
  Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2010/2011 katika haya ya 24 inayohusu shirika la Nyumbu.

  Katika mwaka wa fedha 2009/2010 Shirika la Nyumbu limekamilisha kuandaa mpango
  mkakati wake wa muda mrefu ambao una lengo la kuliganya shirika kuwa kituo maalum cha kuendeleza teknolojia za magari, mitambo ya ndani na nje ya nchi, kufanya utafiti na uzalishaji mdogo mdogo wa bidhaa na vipuri mbalimbali kwa ajili ya sekta za ulinzi na usalama,kilimo, viwanda na usafirishaji,"alisema.

  Alisema kuwa Kambi ya Upinzani ilitegemea kuwa Jeshi la Wananchi lingeingia mkataba kwa ajili ya kuimarisha taasisi ya Nyumbu ili iweze kuzalisha vifaa mbalimbali vitakavyokuwa vinatoa teknolojia rahisi katika mchakato mzima wa uzalishaji wa mazao ya kilimo.

  Bw. Selasini alisema kuwa hiyo sera mpya iliyoletwa na jeshi na kuhalalishwa na
  serikali , yaani jeshi kujiingiza katika masuala ya biashara ya kichuuzi ya kununua kwa mkopo na kuuza, badala ya jeshi kuwa Taasisi, mfano kwa kuvumbua na kusambaza teknolojia katika Nyanja mbalimbali za uzalishaji na hivyo kuinua uchumi wananchi inatia shaka na doa kwa jeshi.

  Alisema kuwa hoja hiyo ya jeshi kutumiwa na baadhi ya wafanyabiashara na matapeli wakishirikiana na baadhi ya Makamanda Wakuu wa Jeshini, imejidhihirisha wazi katika taarifa iliyotolewa na gazeti la kila siku "Dira ya Mtanzania" la Julai 4-6 mwaka huu.

  Bw. Selasini alisema kuwa kutokana na hali hiyo Kambi ya Upinzani imeitaka serikali kutoa taarifa ya kina kuhusiana na taarifa hiyo na ni hatua gani za kinidhamu zimechukuliwa kwa Maofisa hao wa jeshi.

  Alisema kuwa taarifa hiyo ni mwendelezo wa taarifa ambazo zilikwisha lalamikiwa na jamii jinsi ambavyo Bw. Visran Sileshi alivyokuwa akifanya biashara haramu na baadhi ya makamanda wa jeshi na mwisho ilikuwa kwa jeshi kununua vifaa vibovu kwa bei kubwa sana.

  Msemaji huyo wa kambi ya upinzani aliongeza kuwa kwa hali ya kawaida kuna wananchi ambao kutokana na utundu wao wa asili wanatengeneza silaha kama magobore, lakini badala ya jeshi kuwachukua wananchi hao na kuwaendeleza, serikali inawafungulia mashtaka .

  Alisema hali hiyo ni kuwafanya wananchi wenye uwezo wa kubuni na kutengeneza baadhi ya vifaa kuogopa na hivyo vipaji vyao kupotea kabisa jambo ambalo alidai kuwa ni hatari kwa Taifa dogo kama Tanzania.

  Bw. Selasini alisema kuwa usiri ambao unaendelea katika miradi , kampuni ya jeshi umeendelea kuitia hasara nchi, kwani Kambi ya Upinzani kwa miaka mitano iliyopita imekuwa ikihoji umiliki wa mgodi wa meremeta na serikali imeshindwa kutoa majibu sahihi,ambapo Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda aliamua kulieleza Taifa kuwa Meremeta ni suala la ulinzi na usalama na hivyo ni siri na hakuna mtu mwenye uwezo wa kuhoji tena na mjadala ulifungwa.

  "Usiri huu umewaacha wananchi wa Buhemba ambao hadi muda huu bado walikuwa na madai mbalimbali dhidi ya kampuni hiyo ya Meremeta . Kambi ya Upinzani inasema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ni ya kibiashara na hivyo bado tuna haki kabisa ya kuendelea kuhoji ubadhirifu wote uliofanywa na baadhi ya watendaji jeshini kwa mgongo kuwa kila jambo ambalo liko chini ya jeshi ni siri na hakuna mamlaka ya kohoji jinsi linavyoendeshwa,"alisema.

  Alisema kuwa kuna usemi unaosema kuwa "no taxation without representation" kama
  ulivyotolewa na Katibu Mkuu wa Inte-Parliamentary Union, Bw. Anders John pamoja na Mkurugenzi wa Geneva Center for Democratic control of armed forces, Balozi Dkt. Theodor Winkler.

  Bw. Selasini alisema kama bunge linapitisha fedha za walipa kodi kwa matumizi ya taasisi za jeshi, ni lazima wawakilishi wa wananchi ambao ni wabunge waelewe nini kinafanyika na wawe na mamlaka ya kuhoji matumizi ya fedha hizo.

  "Hivyo basi kaulia aliyotoa Waziri Mkuu bungeni kuwa suala la Meremeta limefungwa na halitakiwi kuhojiwa tena kwa kuwa ni siri ya jeshi halina mashiko na ni utetezi dhaifu, kwani kumbukumbu zinaonyesha kuwa kampuni hiyo ya jeshi ilianzishwa kwa fedha za wananchi na wabunge ni wawakilishi wa wananchi.

  Bw. Selasini alisema kuwa pia kumekuwepo na matumizi mabaya ya vifaa vya jeshi kwa matumizi ya kisiasa na binafsi ya wanasiasa, jambo ambalo limeendelea kuongeza gharama kwa jeshi hilo na kwamba mifano hai ni mwaka juzi zilitolewa taarifa za kuanguka kwa helikopta ya jeshi mkoani Manyara iliyokuwa imebeba wazungu waliokuwa kwenye ziara binafsi kwa idhini ya ya Waziri wakati huo Professa Juma Kapuya.

  Alitoa mfano mwingine ni ule wa juzi, ambapo ndege ya jeshi ilitumika kumsafirisha Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw, Freeman Mbowe kwenda Arusha kutekeleza amri ya mahakama na ndege hiyo ilirudi ikiwa na rubani pekee , kwamba hayo ni matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa na halikubaliki.

  Bw. Selasini alisema kuwa Kambi ya Upinzani inaamini kwamba kwa njia ya utunzi wa sera na sheria za ulinzi zitakazotungwa zitakuwa zimewahusisha wanachi kwa kiasi kikubwa na zitasaidia kuondoa migongano isiyokuwa na tija kati ya jeshi na wananchi ikiwa ni pamoja na kuondoa kabisa matumizi mabaya ya askari wa jeshi katika kushughuli za kisiasa kama ambavyo imekuwa ikijitokeza katika hatua mbalimbali za mchakato wa uchaguzi.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sasa Wakirudisha JKT, hao vijana watakuwa wanawafanyia kazi Mafisadi walioingia Mkataba na JKT? There is nothing free anymore in Tanganyika? Everywhere there is some % g belonging to CCM fisadis... Lets see after 2015
   
Loading...