Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,722
Wanabodi,
Hakuna ubishi kuwa kitu chenye nguvu kuliko kitu chochote kwenye mwili wa binaadamu, ni "will power!" yaani nguvu ya nia!.
Ukiweka nia kimoyo moyo kuwa utafanya jambo fulani bila kutamka kwa kauli, hapo itaitwa umenuizia, ila Ukiweka nia kimoyo moyo kisha ukaitamka, tamko hilo linaitwa nadhiri!. Ni lazima ulitekeleze vinginevyo!, you'll have to pay tena hapa hapa duniani!.
Nimesema hivyo kufuatia ukweli kuwa kauli huumba!. Mungu, ameuumba ulimwengu na vyote vilivyomo kwa kauli tuu, alipotamka, na liwe giza, na uwe mwanga, na uwe nchi na yawe mali, etc, na vyote vikawa!. Baada Mungu kuumba kila kitu, akasema na tumuumbe mtu kwa mfano wetu, akafinyanga udongo akamuumba binaadamu na kumpulizia pumzi ya uzima yenye uwezo wa Mungu na kumpa jina la Adam. Hivyo sisi binaadamu tuna uwezo wa Mungu wa uumbaji kupitia kauli, hivyo nasema pasi shaka, maneno au kauli huumba!, hivyo natoa wito tuwe makini sana na kauli zetu tunazotoa na kuwa makini zaidi na nadhiri!.
Miongoni mwa nadhiri za hatari kabisa ni zile nadhiri zinazotolewa mbele ya Mungu , kikiwepo kiapo cha ndoa, au zile nadhiri zinazotolewa mbele ya Mungu kwa mtu kwa kutoa nadhiri kuwa atamtumikia Mungu katika useja, lakini kwa sababu zozote zile akaenda kinyume cha nadhiri yake, inasemekana, kile kiapo na nadhiri ile itamuwinda siku zote za maisha yake, kwa maisha yake kuparaganyika na kwamba s/he will never settle!.
Swali ni Jee kuna ukweli wowote katika hoja hii?. Naomba hebu fuatilia maisha ya watu waliokiuka viapo vya ndoa zao, reflect maisha yao, hali kadhalika fanya reflection ya maisha ya wengine wowote waliokiuka nadhiri zao mbele ya Mungu, maisha yao yakoje ?!. Jee ni kweli yameparaganyika?!. Jee ni kweli maneno huumba?!.
Nawatakieni Jumamosi Njema!.
Wasalaam
Pasco.