muongozaji
JF-Expert Member
- Oct 9, 2009
- 1,386
- 1,000
Habari ya Jumapili WanaJF wenzangu!
Naomba tushee hii light moment pamoja.
Kwanza nikiri kuwa mimi nimekuwa mhudhuriaji mzuri sana wa JF na ni miongoni mwa watu waliofaidika sana kutoka kwenye jukwaa hili. Hata kabla ya kuwa member rasmi wa JF nilikuwa nikiingia kama guest. Udhaifu wangu tu ni kuwa huwa sio mtu wa ku-post sana. Bali mimi ni msomaji mzuri tu humu.
Narudi kwenye mada. Gwiji la mapenzi kwa tafsiri yangu isiyorasmi ni kuwa ni mtu ambaye ni mtaalam (expert) au nyota (star) katika nyanja ya mapenzi. Na sifa kubwa ni kwamba mtu huyu (awe ni me au ke) anawajua vizuri viumbe wa jinsia nyingine kiasi kwamba neno kuumizwa (pain au kuwa heartbroken) kwenye mapenzi ni kitu ambacho hakiwezi kumtokea kamwe. Yeye anazisikia habari hizo kutoka kwa watu wengine na kwamba anawashangaa sana. Wakati mwingine anawaona ni wajinga fulani au malimbukeni wa mapenzi.
Nimesukumwa kuandika hii thread kutokana na observations zangu humu JF MMU. Sitaki kutaja majina kwasababu list ni ndefu lakini kuna wana JF ambao ni icons kwenye kutoa ushauri unaohusiana na ishu za kimahusiano/mapenzi. Wengi tumefaidika kutoka kwao.
Wapo hao WanaJF waliowabeza na kuwadhihaki wale watu waliopost hapa kuomba ushauri kutokana na maumivu ya mapenzi waliyokuwa wanayapitia. Baadhi ya reactions za wanaJF hao zilikuwa zina-project ujumbe kuwa wao ni magwiji wa mapenzi na wanashangaa kwanini mtu uumizwe na mapenzi kama sio ujinga wa kujitakia.
Wale waliokuja hapa wanalialia wamekuwa wakiambiwa hawana uzoefu wa kutosha kwenye mapenzi, wanapenda kijinga, hawako makini kwenye kufanya maamuzi, wanaburuzwa na hisia, watumwa wa mapenzi etc etc.
Mimi kwa kiasi kikubwa naamini kila mtu has a huge potential ya kuumizwa. Inategemea tu kwamba amekuwa akitengeneza mahusiano ya aina gani na watu wa aina gani na kwa wakati gani!! Kikubwa ni kwamba anakuwa amependwa au amependa kwa kiasi gani? Msimamo wangu binafsi ni kuwa kila mtu ana nafasi ya kuumizwa na mapenzi na kwamba uzoefu wa mtu haumpi kinga ya kuumizwa zaidi ya kuwa tu na utajiri wa mbinu za kuchukua tahadhari ili asinase kirahisi.
Naomba WanaJF wenzangu mjitokeze mtoe ushuhuda na uzoefu wenu kuhusu hili suala. Je, wewe binafsi unaamini kwa uhakika kabisa kuwa kuna watu hawawezi kuumizwa katu au kutetereshwa na dhoruba la mapenzi kabisa? Je kuna magwiji wa mapenzi?
Unaweza kutoa mtazamo wako kwa kujitathmini wewe mwenyewe au uzoefu wako kwa kuona kwa watu wengine.
Nasubiria kusoma kutoka kwa wale "magwiji wa mapenzi". Itafaa pia kama tutaelimishana ili tuzijue mbinu za kumuwezesha mtu kuepuka kuumizwa katika mapenzi.
Asanteni wadau.....