Je, Wewe ungejibu nini?

47pro

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
1,204
332
Kama mtu akikuuliza swali lifuatalo; Kwanini unampenda mke wako au mume wako au mchumba wako, utampa jibu gani? Wanaume wengi (siyo wote) katika kujibu hili swali wanaweza kujikuta wanajibu nampenda mke wangu kwa sababu ana sura nzuri, au ana mguu wa nguvu, au ana macho mazuri au ana umbo zuri au ana nywele nzuri au ana kifua kizuri (matiti) au kwa sababu ni mwimbaji mzuri au kwa sababu wazazi wake ni matajiri, au anapika vizuri nk.

Wanawake nao wanaweza kujikuta wanajibu kwa kuwapa sifa za uhakika waume zao kama vile ninampenda kwasababu amesoma, nampenda kwasababu ni handsome, nampenda kwa sababu ana kazi nzuri au ana fedha au kwasababu amesoma au kwasababu anakuwepo pale ninapomuhitaji.

Je, utakuwaje kama baada ya miaka mingi kupita na mume wako au mke wako akabadilika vile vitu ambavyo vilikuwa ndiyo msingi wa wewe kumpenda? Je, utaendelea kumpenda? Kutokana na ulivyojibu swali hapo juu, Na Kama una akili timamu (logically) jibu linatakuwa huwezi kumpenda tena mke wako au mume wako kwani msingi wako wa kumpenda umeshatoweka.

Kama sababu za kumpenda mume wako au mke wako zina msingi katika qualities ambazo baada ya muda zinaweza kubadilika au kupotea hii ina maana msingi wa kumpenda pia hupotea (love will be over) Ukweli ni kwamba njia sahihi na kamili ya kupenda mke au mume ambayo huweza kudumu maisha yote ni kumpenda kama alivyo (unconditional love) au kuchagua kumpenda kama alivyo. “Love is not a feeling; it is a choice and commitment” Kuna aina tatu muhimu za upendo ambazo huweza kusaidia wawili wanaopendana kudumu; nazo ni upendo wa Agape (true love), pili ni (Phileo) upendo wa urafiki na tatu (Eros) upendo wa kimahaba.

Hata hivyo upendo wa msingi ambao huwawezesha mke na mume kuishi pamoja miaka yote na kushinda yote katika hali zote ni upendo wa Agape. Upendo wa urafiki (phileo) na upendo wa kimapenzi (Eros) ni muhimu katika ndoa hata hivyo kama ndoa yako ina msingi au imesimamia katika aina hizi mbili (Phileo & Eros) au kufurahia urafiki na mapenzi (sex life) tu basi ndoa au mahusiano yako yamejengwa juu ya mchanga. Upendo unaojenga ndoa ni ule usio na ubinafsi, usio na sababu au masharti (selfless/ unconditional) ambao ni Agape. Huu ni upendo ambao kuchakaa kwa mwili au kubadilika kwa hali za maisha hakuwezi kutikisa ndoa.

Huu ni upendo ambao huweza kuwapitisha wanandoa katika ugonjwa na afya njema, umaskini na utajiri, katika mazuri na katika mabaya, katika giza na katika nuru ni upendo ambao ni true love. Ni upendo ambao hata mume akiota kitambi bado mke atampenda, ni upendo ambao hata mke akinenepa na kuwa na kilo 300 bado mume atampenda na kujiona fahari nk.

Ikitokea mume akamwambia mke wake “sina feelings na wewe tena” hii ina maana anasema kwamba “sikukupenda kama ulivyo, bali wakati nakuoa nilikupenda kwa sababu ulikuwa na sura nzuri na sasa umesinyaa usoni ndiyo maana sikupendi, nilikupenda kwasababu ulikuwa na matiti mazuri na sasa yamelala ndiyo maana sikupenda, nilikupenda kwasababu ulikuwa portable na sasa umenenepa kama elephant ndiyo maana sina feelings na wewe.

Upendo wake ulikuwa na msingi wa feelings na circumstances na si commitment, hakuchagua kumpenda mke wake bali alijisikia kupenda kutokana na mwonekano au Urembo na si kuchagua kumpenda kama alivyo. Naamini ukiulizwa kwanini unanipenda hutajibu.
 
Lazima kutakuwa na sababu iliokuvutia juu ya mwenza wako ila ukiwa nae unaendelea kuongeza kuvutiwa na mengine juu yake. Ikifikia kukipoteza kile ulichokipenda mwanzo basi vingine bado vipo vilivyokuvutia kwake.
 
Mmmmmmmmmmmmmmmmh ngoja nijipitie zangu tuwaache na malove ya wanadamu, ila ni upendo wa Mungu t usio kuwa na mipaka wala haungalii hali uliyokuwa nayo
 
Utasema ulichompendea,kama moyo wake,tabia yake,michezo yake,pesa zake,anavyokujali wewe na watu wako sababau ni nyingi sana...
 
Mkuu hujamaliza dissertation yako?? Naogopa kuchangia mada zako isije kua nakupa data bila bila kujua!!!
 
Nimempenda kwa sababu nampenda...for better for worse nipo nae....For ups for downs tupo pamoja...Thats all!!!
 
Sina sababu ya kumpenda huyu mtu. I just love him...kwa mazuri yake nampenda..kwa mabaya yake nampenda..kwa kuvutia kwake nampenda..kwa kuchukiza kwake nampenda..kwa utajiri wake nampenda...kwa umasikini wake nampenda. I just cant explain why i love him. Love yangu kwake ndio hivyo yaani!
 
Sina sababu ya kumpenda huyu mtu. I just love him...kwa mazuri yake nampenda..kwa mabaya yake nampenda..kwa kuvutia kwake nampenda..kwa kuchukiza kwake nampenda..kwa utajiri wake nampenda...kwa umasikini wake nampenda. I just cant explain why i love him. Love yangu kwake ndio hivyo yaani!
Asante kwa kunipenda mwaya!
 
mmemaliza kupendana na muelewe bongo hakuna love ulaya kwa mapenzi ndio mambo yote maana mnapendana mkiwa wadogo had I mnakuja kuoana na sio bongo siku mbili mnazinguana tayari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom