Je, wanadai demokrasia yao kimyakimya?

Je, wanadai demokrasia yao kimyakimya?

Mchokoo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
1,188
Reaction score
1,604
Hivi yawezekana hii ikawa ni hulka ya ya watu wa taifa hili?
Kwamba, watanzania hawakuchukua silaha kukabiliana na watawala wa kikoloni katika kudai uhuru wao, bali waliipigania haki yao kimyakimya bila sauti ya mtutu kusikika.

Hata Mzee Mandela alipomjulisha Mwalimu juu ya azma ya ANC kuchukua silaha dhidi makaburu, bado mzee wetu hakuukubali mpango huo!
Sasa ninapouona uchache wa kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura; najiuliza, je, huku ndiko kudai haki hii nayo kimyakimya?

Haki ya uhuru wa kujiamulia mambo. Uhuru wa kuchaguana, kuchagua, na kuchaguliwa.
Eti labda ndiyo imesababisha watu wengi wameacha kwenda kujiandikisha kama wanavyosema baadhi ya wadau.
Kama si sababu nyingine iliyopelekea; sasa yawezekana wabongo wakayafundisha mataifa mengine kwamba; kudai chako sio lazima ufanye magomvi?

Wadau hili mnalionaje?
 
Hayo ni mawazo yako na mawazo yako ni yako sio ya wote, usifikirie mawazo yako ni ya wote.

Binafsi mpaka leo sijajiandikisha ila leo ntajiandikisha na nashukuru Serikali kwa kuongeza muda maana Watanzania wa sasa wapo bize na kazi.
 
Wewe wasema mawazo yangu ni ya wote! Haya ni mawazo yako ambayo si ya kwangu pia.
Hayo ni mawazo yako na mawazo yako ni yako sio ya wote, usifikirie mawazo yako ni ya wote.

Binafsi mpaka leo sijajiandikisha ila leo ntajiandikisha na nashukuru Serikali kwa kuongeza muda maana Watanzania wa sasa wapo bize na kazi.
 
Mkuu serikali inabidi ijipime upya kuhusu kuikuza na kuiishi demokrasia kwa vitendo. Jana kuna mama mmoja alikuwa anamuuliza jamaa mmoja hivi yule mama sikumbuki vizuri kama ni mkuu wa wilaya au ni mkurugenzi huko Tanga.

Alimuuliza jamaa kama alishajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura jamaa akasema haoni umuhimu kwa sababu kila siku mambo ni yale yale tu. Huyu hakufunga mambo ni '' yale yale'' hayo ni mambo gani?

Ukute watanzania wengi wameshachoka kugeuzwa wajinga kwa mfumo huu wa sasa hivi. Serikali hata ifanye mazuri kiasi katika dunia ya leo haiwezi kukubalika 100% na wananchi wake hivyo kitendo cha mkuu wa nchi na chama tawala kusimama kusema watashinda kwa kishindo na kutoa hizi takwimu zao ndio kitu kina wachosha na kuwarudisha nyuma watanzania.

Mfano mdogo ni huyu katibu mwenezi wa chama tawala anadai chama chake kimevuna wanachama milioni 15 na huku waziri wa TAMISEMI anasema watarajia kuandikisha wapiga kura milioni 26 kwa hesabu za kawaida tu hapo unahisi kuna dalili ya upinzani kushinda mtaa au kata yoyote.

Wacha wapeane hizo kura zisizopigwa na watu bali ni zile walizopiga wenyewe ndio zitawapa ushindi.
 
Hayo ni mawazo yako na mawazo yako ni yako sio ya wote, usifikirie mawazo yako ni ya wote.

Binafsi mpaka leo sijajiandikisha ila leo ntajiandikisha na nashukuru Serikali kwa kuongeza muda maana Watanzania wa sasa wapo bize na kazi.
Wako bize na kazi eeeh! kwa hiyo miaka mingine hawakuwa na kazi sasa awamu ya 5 imeleta kazi kwa kila raia wa 18+?
 
1. passive reaction ya wabongo kujiandikisha.

2. wakulima wa korosho, pamba, nk.

3. watumishi kuzimwa stahili zao kimwamba.

4. akijiongeza hata nusu saa ya kushika usukani

5. akithubutu kumkabizi fala bashite aka konda kusogelea usukani.

hapo ndipo atajua kuwa tz ina historia yake tofauti duniani.
 
Hayo ni mawazo yako na mawazo yako ni yako sio ya wote, usifikirie mawazo yako ni ya wote.
Binafsi mpaka leo sijajiandikisha ila leo ntajiandikisha na nashukuru Serikali kwa kuongeza muda maana Watanzania wa sasa wapo bize na kazi.
Huku ni kupanic na roho kukuuma duh
 
Hayo ni mawazo yako na mawazo yako ni yako sio ya wote, usifikirie mawazo yako ni ya wote.
Binafsi mpaka leo sijajiandikisha ila leo ntajiandikisha na nashukuru Serikali kwa kuongeza muda maana Watanzania wa sasa wapo bize na kazi.
!!!!???????!!!!!!!!ABRACADABRA
 
Hayo ni mawazo yako na mawazo yako ni yako sio ya wote, usifikirie mawazo yako ni ya wote.
Binafsi mpaka leo sijajiandikisha ila leo ntajiandikisha na nashukuru Serikali kwa kuongeza muda maana Watanzania wa sasa wapo bize na kazi.
Awamu hii kwa kujipa ujiko hamjambo. Kwa hiyo awamu zilizopita wananchi hawakuwa bize na kazi?!
 
Hivi yawezekana hii ikawa ni hulka ya ya watu wa taifa hili?
Kwamba, watanzania hawakuchukua silaha kukabiliana na watawala wa kikoloni katika kudai uhuru wao, bali waliipigania haki yao kimyakimya bila sauti ya mtutu kusikika.

Hata Mzee Mandela alipomjulisha Mwalimu juu ya azma ya ANC kuchukua silaha dhidi makaburu, bado mzee wetu hakuukubali mpango huo!
Sasa ninapouona uchache wa kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura; najiuliza, je, huku ndiko kudai haki hii nayo kimyakimya?

Haki ya uhuru wa kujiamulia mambo. Uhuru wa kuchaguana, kuchagua, na kuchaguliwa.
Eti labda ndiyo imesababisha watu wengi wameacha kwenda kujiandikisha kama wanavyosema baadhi ya wadau.
Kama si sababu nyingine iliyopelekea; sasa yawezekana wabongo wakayafundisha mataifa mengine kwamba; kudai chako sio lazima ufanye magomvi?

Wadau hili mnalionaje?
Hali ngumu ya maisha watu wakiamka wana waza watakula nini leo wapo bize kutafuta riziki
 
Back
Top Bottom