Je! wajuwa kuwa maisha unayoishi ndiyo Ibada?

twijuke

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
547
252
Dini zote tumeaswa katika katika upendo, lakini tumejawa na ubinafsi, mfano unaingia ndani ya chumba cha wagonjwa kumjulia hali mgonjwa wako, lakini kwa ubinafsi unamjulia hali mgonjwa wako tu na unaondoka zako, unasahau kuwa hata hao wengine hata kama hamjuani wanahitaji pole yako. Je! wajisikiaje u mgonjwa kitandani mtu hakujui anakupa pole? ni ukweli usiopongika na inatia sana faraja mtu hakujui kukupa pole.

Unapita njia nyembaba unaona kigae cha chupa na unakiacha, na badaye kumchoma mpita njia mwingine, kumbe unge kiondoa na kukirusha mbali ungemwokoa, hii ni mifano midogo tu kwamba ibada ni maisha haya tunaoyoishi kilasiku. Kushinda makanisani na misikitini huku tukimlilia Mungu kwa haja ya mioyo yetu, kama hatutendi mema sala zetu mbele ya Mungu naamini ni bule.

Angalizo katu simaanishi tusiende makanisani na misikitini ..hapana.. bali namaanisha tunayo fundishwa kuko tuyaishi.
 
Dini zote tumeaswa katika katika upendo, lakini tumejawa na ubinafsi, mfano unaingia ndani ya chumba cha wagonjwa kumjulia hali mgonjwa wako, lakini kwa ubinafsi unamjulia hali mgonjwa wako tu na unaondoka zako, unasahau kuwa hata hao wengine hata kama hamjuani wanahitaji pole yako. Je! wajisikiaje u mgonjwa kitandani mtu hakujua anakupa pole? ni ukweli usiopongika na inatia sana faraja mtu hakujui kukupa pole.

Unapita njia nyembaba unaona kigae cha chupa na unakiacha, na badaye kumchoma mpita njia mwingine, kumbe unge kiondoa na kukirusha mbali ungemwokoa, hii ni mifano midogo tu kwamba ibada ni maisha haya tunaoyoishi kilasiku. Kushinda makanisani na misikitini huku tukimlilia Mungu kwa haja ya mioyo yetu, kama hatutendi mema sala zetu mbele ya Mungu naamini ni bule.

Angalizo katu simaanishi tusiende makanisani na misikitini ..hapana.. bali namaanisha tunayo fundishwa kuko tuyaishi.

Gooood!
 
wengi wetu hitaji letu mbele ya Mungu ni haja ya mioyo yetu,mali,mtoto,magonjwa, na mambo mengine mengi. Hvyo ndo maana hatuishi maisha ya kumpendeza Mungu.
 
Kwa hilo la kwenda hospitalini na kumpa mgonjwa anayenihusu tu pole, Mungu anisamehe kwa hilo, Nashukuru mleta mada kwa kunionyesha dhambi niliyokuwa naitenda bila kujua
 
Mleta maada nafikiri atakuwa mchungaji au shehe. Mi namshukuru Mungu kwa upeo mzuri na huruma alonipa juu ya hayo na mengineyo. Ubarikiwe sana.
 
Wako watu hawaendi misikitini na makanisani, lakini mfumo wa maisha wanayoishi ni wa kumpendeza Mungu. ubinafsi umetuzidi, mtu hasemi sisi bali anasema mimi, haya ndo yanatokea kwa watawala wetu wanajifikiria wao kwanza.
 
Na hiyo tabia inaanzia kwenye malezi, too bad!
 
Nikweli na mambo yanaelekea kubaya zaidi hasa hiki kizazi cha .com
 
Dini zote tumeaswa katika katika upendo, lakini tumejawa na ubinafsi, mfano unaingia ndani ya chumba cha wagonjwa kumjulia hali mgonjwa wako, lakini kwa ubinafsi unamjulia hali mgonjwa wako tu na unaondoka zako, unasahau kuwa hata hao wengine hata kama hamjuani wanahitaji pole yako. Je! wajisikiaje u mgonjwa kitandani mtu hakujui anakupa pole? ni ukweli usiopongika na inatia sana faraja mtu hakujui kukupa pole.

Unapita njia nyembaba unaona kigae cha chupa na unakiacha, na badaye kumchoma mpita njia mwingine, kumbe unge kiondoa na kukirusha mbali ungemwokoa, hii ni mifano midogo tu kwamba ibada ni maisha haya tunaoyoishi kilasiku. Kushinda makanisani na misikitini huku tukimlilia Mungu kwa haja ya mioyo yetu, kama hatutendi mema sala zetu mbele ya Mungu naamini ni bule.

Angalizo katu simaanishi tusiende makanisani na misikitini ..hapana.. bali namaanisha tunayo fundishwa kuko tuyaishi.

Sawa nimeerewa
 
Umetukumbusha kitu kizuri, haya ndio mambo yanayotakiwa JF hasa jukwaa la MMU.

Naomba tu niongezee andiko hapo..

"Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,

mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo."

Wakolosai 3:23-24
 
  • Thanks
Reactions: len
Yes...baada ya tafakuri hii ya twijuke nimepata wazo moja.....dunia ya sasa inaangamizwa na dhambi moja kubwa......UBINAFSI......hebu fikiri matatizo yoyote ya ulimwengu na walimwengu wa sasa kama chagizo kuu halitakuwa UBINAFSI.......
 
Last edited by a moderator:

Mi nafikiri dhambi hii ya ubinafsi inaitafuna Tanzania kuliko nchi yeyote.

Laiti viongozi wetu wangeishi amri kuu ya mapendo, ufisadi huu tunaoushuhudia tusingeuona.

Mfano ni yule wakili wa Tanesco aliyechukua mamilioni huku akijua anachangia gharama za umeme kupanda. Mtu huyo huyo anajifanya anaupendo kwa kwenda kujenga mashule jimboni mwake. Kuna mwingine ki ujanja ujanja amechukua mabilioni kutoka account ya IPTL, sijui anajiita VIPI? baadae anajifanya msamalia mwema kudhamini wasanii na mbio za mwenge.

Watu wakiishi imani, ufisadi utapungu!
 
Last edited by a moderator:
Yes...baada ya tafakuri hii ya twijuke nimepata wazo moja.....dunia ya sasa inaangamizwa na dhambi moja kubwa......UBINAFSI......hebu fikiri matatizo yoyote ya ulimwengu na walimwengu wa sasa kama chagizo kuu halitakuwa UBINAFSI.......

Ni kweli kabisa, wizi, ufisadi, dhuluma, uongo, nk yote ni matokeo ya ubinafsi tu
 
Shule za st Kayumba vs Academy ni UBINAFSI.......Hadi uzinzi ni tunda la UBINAFSI..........
 
Mwana Jf mwenzangu, Ndg Mtazamo, kuna wakati inanipelekea kuamini kuwa CCM hawaamini katika Mungu, "ebu check matendo yao"
 
Back
Top Bottom